Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WATOA ANGALIZO KWA MADEREVA,WAPONGEZA JUHUDI ZA PUMA ENERGY TANZANIA

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WATOA ANGALIZO KWA MADEREVA,WAPONGEZA JUHUDI ZA PUMA ENERGY TANZANIA

pu1

Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti,akizungumza na waandishi wa habari  katika uzinduzi wa mafunzo  ya Usalama barabarani kwa nafunzi wa mkoa wa Dar es Salaam,na Luvuma.

pu2

Mshindi wa mchoro 2017, mwanafunzi wa darasa la sita shule ya Msingi Mbande, Nasri Mustafa, akiwaonyesha  mchoro wake wa usalama barabarani alioshindawakati wa uzinduzi wa mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam jana, kutoka kulia, Meneja Miradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend, Simon Kalolo, meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, trafki kutoka makao makuu, ASP Mbuja Matibu na Sajent Hussein Ramadhani

pu3

trafki kutoka makao makuu, ASP Mbuja Matibu akinzumgumza na waandhi wa habari katika uzinduzi wa mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi mkoa ya Dar es Salaam,Ruvuma

pu6 pu7

Walimu na wanafunzi pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar as Salaam.

pu8

Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti,trafki kutoka makao makuu, ASP Mbuja Matibu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali leo jijini Dar as Salaam.

………………………………………………………………………………………………………………

NA MWANDISHI WETU

POLISI Kikosi cha Usalama Barabarani imewataka madereva na watumiaji wa barabara kuacha kukariri badala yake wahakikishe wanazingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali.

Pia, imepongeza kuongezeka kwa uelewa miongoni mwa watumiaji wa barabara husuani katika kuzingatia matumizi ya vivuko vya watembea kwa miguu.

 Akizindua Mpango wa Usalama Barabarani wa Puma Energy Tanzania Mwaka 2018, Mwakilishi wa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Mbunja Matibu, alisema madereva na watumiaji wote wa baraba hawapaswi kukariri alama za barabari.

Mrakibu Matibu alisema ili kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya barabara kila mtumiaji wa barabara anapaswa kuwa makini muda wote kwani kwa kufanya hivyo anaweza kutambua hata pale kunapofanyika mabadiliko kwenye sehemu mbalimbali za barabara.

“Usikariri kuwa sehemu ile huwa kuna kibao kinachoelekeza mwendo stahili au eneo la kivuko cha watembea kwa miguu, kunaweza kufanyika mabadiliko ambayo bila ya kuwa makini utajikuta unavunja sheria,”alisema.

Hata hivyo alisema kumekuwepo na ongezeko la uwelewa miongoni mwa watumiaji wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu na madereva jambo ambalo ni la kupongezwa.

Sehemu mbalimbali hususani Dar es Salaam hivi sasa ukitembe utakuta madereva wakisimamisha vyombo vyao kwenye alama za pundamilia ili kuruhusu watembeo kwa miguu waweze kupita. Jambo hili na la kupongezwa na kuendelezwa.

Kwa upande wake Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema kampuni hiyo inatambua na kuthamini umuhimu wa kuwaelermisha watoto kuhusu sheria za ulama barabarani ndio maana imekuwa ikiendesha mpango huo kila mwaka na kuwafikia watoto wengi walioko shuleni.

Corsalleti alisema Puma Energy itaendelea na utaratibu huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo kampuni ya Amend kuhakikisha elimu zaidi inatolewa na Watanzania hususani wanafunzi waliko shule za msingi wanafikiwa.

 Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Amend, Simon Kalolo, alisema lengo la kushirikiana na Puma kutekeleza mpango huo ni kuhakikisha wanajenga uelewa wa matumizi sahihi ya barabara ahatua ambayo itapunguza ajali za barabarani.

Kalolo alisema kampuni yao inaendesha mpango huo kwa mwaka wa sita hapa nchini na kwamba wanafanya hivyo katika nchi tisa Afrika ili kuondoa ajali za barabarani.

Awali akieleza madhumuni ya mpango huo, Neema Swai kutoka Amend, alisema mwaka 2018 utashirikisha mikoa ya Dar es Salaam na Ruvuma ambapo zaidi ya shule 22 zitahusika  ambapo kutatolewa elimu, kuendesha mashindano ya uchoraji na kutoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuongeza uelewa kwa wanafunzi na walimu kuhusu usalama barabarani.

About bukuku

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

19 − ten =