Wednesday , January 16 2019

Home / BIASHARA / BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha leo ,kuhusu mkutano mkuu wa ishirini na tatu wa Wanahisa unaotarajia kuanza rasmi tatehe 18 na 19 utakaohudhuriwa na wanahisa zaidi ya Elfu moja  katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC uliopo jijini Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei kushoto,kulia ni Mkurugenzi wa mikopo James Mabula  kulia 

Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa masoko wa CRDB Jadi Ngwale,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei
Waandishi wa habari wakiwa wanafanya mahojiano ya kina kuhusu mkutano huo 


Na Pamela
Mollel,Arusha
 
Benki ya
CRDB inatarajia kufanya mkutano wake wa ishirini na tatu(23)wa wanahisa wa
benki hiyo katika ukumbi wa Kimataifa wa AICC ulipo jijini Arusha na
kuhudhuriwa na watu zaidi ya Elfu moja.
 
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei
alisema kuwa mkutano huo wa wanahisa unatarajiwa kufanyika tarehe 19 mwezi
huu
 
Dkt.Kimei
alisema kuwa Mkutano huo wa wanahisa wa benki ya CRDB utatanguliwa na semina
maalumu kwa wanahisa wa benki hiyo utakaofanyika tarehe 18 mwenzi huu ambapo
pamoja na mambo mengine wanahisa watapata fursa ya kufahamu mambo mbalimbali kibenki
 
Alisema kuwa
agenda za mkutano huo ni kupokea na kupitisha taarifa za fedha na ripoti za
wakurugenzi kwa mwaka uliopita tarehe 31 mwezi Disemba 2017,kuhidhinisha
taarifa maalumu ya gawiyo wa mwaka ,kuchagua wajumbe wa bodi ,kuhidhinisha
uchaguzi wa wakaguzi wa hesabu wanaokupalika kisheria
 
Dkt Kimei
alitoa rai kwa wanahisa wa benki hiyo kuuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo
mkuu huku akiongeza kuwa kwa mwanahisa ambaye hataweza kuudhuria anahaki ya
kuchagua mwakilishi au wawakilishi kuudhuria na kupiga kura kwa niaba yake
Mwisho.

 

About Alex

Check Also

PICHA 1

TRA YAKUSANYA TRILIONI 7.9 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 6 YA MWAKA WA FEDHA 2018/19

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × three =