Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe afanya ziara ya kushitukiza kwenye maghala ya kuhifadhia Mafuta ya kula

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe afanya ziara ya kushitukiza kwenye maghala ya kuhifadhia Mafuta ya kula

index

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe, leo Mei amefanya ziara ya kushitukiza  kupita kwenye maghala ya kuhifadhia Mafuta ya kula na sukari katika Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kukagua wafanya Biashara wanaoficha bidhaa hiyo.

DK. Kebwe amefanya ziara hiyo leo  Mei 15 akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo na kujionea maghala mengi yakiwa na mafuta ya kula na kuwataka wafanyabiashara hao kupeleka sokoni mafuta hayo na kuuza kwa bei elekezi ya Serikali.

Hata hivyo DK. Kebwe amekemea vikali kitendo cha wafanyabiashara hao kuchanganya biadhaa za chakula kama mafuta ya kula na sukari na bidhaa nyingine kama sabuni chumvi n.k zikiwa ghalani kwa kuwa kufanya hivyo kunahatarisha afya ya walaji.

Katika ukaguzi huo DK. Kebwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro na Maafisa wa TRA wa Mkoa huo kumchukua kumchukua na kumhoji Mfanyabishara wa Mafuta ya kula  Hussein Bionzo na kupitia nyaraka zake za biashara ili kujiridhisha iwapo analipa kodi stahiki Serikalini.

Hatua hiyo imekuja baada ya makosa kadhaa yaliyojitokeza wakati zoezi la kukagua bidhaa ya mafuta ya kula katika ghala lake.

Katika hatua nyingine Dk. Kebwe amewataka wananchi wa Morogoro kutokuwa na wasiwasi wowote kuhusu bidhaa ya mafuta kwa kuwa bidhaa hii ipo ya kutosha huku akiwataka Wakuu Wa Wilaya wote katika Mkoa wa Morogoro kupita katika maduka ya reja reja na kusimamia bei elekezi ya mafuta hayo kwani huko ndiko kuna tatizo la kupandisha bei hasa kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani.

About bukuku

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × five =