Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / WAKANDARASI DAR WAMUUNGA MKONO RC MAKONDA KWA KUJENGA MITARO BURE.

WAKANDARASI DAR WAMUUNGA MKONO RC MAKONDA KWA KUJENGA MITARO BURE.

index1 Zaidi ya Kampuni 70 za ukandarasi zimejitolea kujenga mitaro ya barabara mbalimbali za Dar es salaam Bure kama sehemu ya kuunga mkono jitiada za Mkuu wa mkoa huo Mhe. Paul Makonda.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kufanya ziara usiku na mchana na kujionea uharibifu mkubwa wa barabara uliotokana na ukosefu wa mitaro ya maji na kuamua kuwashirikisha wakandarasi ambao walipokea kwa mikono miwili ombi hilo.

RC Makonda amewaagiza wenyeviti wa mitaa kuratibu idadi barabara zisizokuwa na mitaro kwenye mitaa yao kisha kupeleka  kwa Meneja wa TARURA Wilaya kwaajili ya kupatiwa kampuni itakayojenga mitaro hiyo.

Aidha RC Makonda amezishukuru kampuni zilizojitolea kujenga mitaro hiyo Bure jambo litakalosaidia kuokoa mabilion ya pesa za serikali.

Kwa upande wao wakandarasi wamesema wamejiandaa vizuri kuanzia vifaa na wataalamu kwaajili ya ujenzi huo huku baadhi yao wakiwa tayari wameanza ujenzi kwenye baadhi ya mitaa.

index2

About bukuku

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

10 − 9 =