Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / MAMA JANET MAGUFULI AWAKUMBUKA WAFUNGWA GEREZA SEGEREA

MAMA JANET MAGUFULI AWAKUMBUKA WAFUNGWA GEREZA SEGEREA

PIX 1

Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza afande Gaston Sanga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mama Janet Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam  leo kwa ajili ya kupokea msaada wa vyakula vya wafungwa.

PIX 2

Mama Janet Magufuli mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa pili kushoto) akitoa hotuba fupi leo ofisini kwake Ikulu kabla ya kukabidhi vyakula mbalimbali kwa wafungwa wa gereza la Segerea jijini Dar es Salaam. Mama Magufuli ametoa msaada wa sukari tani 2.8, mchele tani 4.8, unga wa mahindi tani 4.8 na tende. Amesema msaada huo  hasa ni kwa wafungwa wa kike, watoto na wale walio katika mfungo wa Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni ishara ya kuwatambua na kuwathamini pamoja na kwamba wako gerezani.

PIX 3

Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza afande Gaston Sanga(wa tatu kulia)  akipokea sehemu ya vyakula kutoka kwa Mama Janet Magufuli (wa pili kushoto). Wa pili kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam (RPO) Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Augustino Mboje na wa kwanza kulia ni Mkuu wa gereza la Segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Widson Mwanangwa

PIX 4

Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza afande Gaston Sanga(wa kwanza kushoto)  akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa vyakula vya wafungwa kutoka kwa Mama Janet Magufuli (wa tatu kulia). Wa pili kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam (RPO) Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Augustino Mboje na wa kwanza kulia ni Mkuu wa gereza la Segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Widson Mwanangwa. Pamoja na shukrani hizo Kaimu Kamishna Jenerali amemtaka RPO Dar es Salaam  na Mkuu wa Gereza Segerea kuhakikisha vyakula hivyo vinatumiwa na wafungwa na si vinginevyo. Aidha, Kaimu Kamishna Sanga ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kutoa misaada mbalimbali kwa wafungwa ikiwa ni ishara ya kuwatambua, kuwathamini na kuwapa tumaini waliopo magerezani kuwa ipo siku watarudi katika jamii zao baada ya kumaliza vifungo au mashauri yao.

PIX 5

Mama Janet Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza waliofika ofisini kwake  kwa ajili ya kupokea msaada wa vyakula mbalimbali alivyovitoa kwa wafungwa wa gereza la Segerea leo.

Picha zote na

Kitengo cha Habari na Mawasiliano

Makao Makuu ya Magereza

Dar es Salaam

About Alex

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nine + 6 =