Tuesday , March 26 2019

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

Msangi3

  • MTOTO AFARIKI DUNIA BAADA YA KULIPUKIWA NA MOTO MDOMONI MITHILI YA UMEME WAKATI AKIUNGANISHA NYAYA ZA RADIO NA BETRII YA SIMU KWA KUTUMIA MDOMO WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 17.05.2018 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI KATIKA MTAA WA IGOMA MASHARIKI JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DOTTO BARAKA JAFARI MWENYE UMRI WA MIAKA 13, MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI SABASABA, AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KULIPUKIWA NA MOTO MDOMONI MITHILI YA UMEME WAKATI AKITENGENGENEZA RADIO CHAKAVU KISHA KUUNGANISHA NYAYA YA RADIO NA BETRII YA SIMU KWA KUTUMIA MDOMO, HALI ILIYOPELEKEA MLIPUKO MKUBWA ULIOSAMBARATISHA MDOMO, TAYA ZOTE, MENO YOTE NA KOO NA BAADAE KUFARIKI DUNIA WAKATI AKIKIMBIZWA HOSPITALI.

AWALI INADAIWA KUWA WAZAZI WA MAREHEMU WALIKUWA SAFARINI KWENDA KAHAMA MKOANI SHINYANGA NA NYUMBANI  WALIBAKI WATOTO. INASEMEKANA KUWA WAKATI MAREHEMU ALIPOTOKA SHULE ALIRUDI NYUMBANI KISHA KUANZA MICHEZO YA KUTENGENEZA RADIO CHAKAVU AKIWA PAMOJA NA WATOTO WENZAKE NJE YA NYUMBA YAO.

INASEMEKANA KUWA WAKATI MAREHEMU AKIENDELEA KUTENGENEZA RAIDO HIYO CHAKAVU, ALICHUKUA BETRII CHAKAVU YA SIMU YA MKONONI YA AINA YA SAMSUNG KISHA ALIIUNGANISHA NA NYAYA ZA MABAKI YA RIDIO CHAKAVU KWA KUTUMIA MDOMO NDIPO GHAFLA ULITOKEA MLIPUKO MKUBWA MDOMONI ULIOSAMBARATISHA MDOMO WOTE, MENO, TAYA NA KOO. WANANCHI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUMKIMBIZA MAREHEMU HOSPITALI, LAKINI ALIFARIKI DUNIA NJIANI.

POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, PIA HUKUNA MTOTO MWINGINE YEYOTE ALIYEPOTEZA MAISHA AU KUJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA POLE KWA FAMILI, NDUGU, JAMAA NA  MARAFIKI KWA MSIBA HUO, MWENYEZI MUNGU AWAPE NGUVU NA UVUMILIVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU WAKATI JESHI LIKIENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO. SAMBAMBA NA HILO PIA ANAWAOMBA WAZAZI WAWE WAANGALIFU NA WATOTO WAO WASIWARUHUSU KUCHEZEA VITU KAMA HIVI AMBAVYO VINAWEZA KUPELEKEA MAJERUHI AU VIFO KWA WATOTO. PIA ANAWAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

 

About Alex

Check Also

AA

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eleven + 5 =