Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / MAJALIWA AFUNGUA SEMINA ENDELEVU YA 29 YA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI JIJINI DODMA

MAJALIWA AFUNGUA SEMINA ENDELEVU YA 29 YA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI JIJINI DODMA

PMO_1274

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Semina Endelevu  ya 29 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu  Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018

PMO_1265

Baadhi ya washiriki wa   Semina Endelevu  ya 29 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu  Majengo na Wakadiriaji Majenzi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua semina hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.

PMO_1258

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza  kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Semina Endelevu  ya 29 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu  Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.

PMO_1157

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mauzo wa Kampuni ya  Locks and Systems Limited ya Dar es salaam, Linda Mwamukonda kuhusu vitasa, bawaba na milango ya kielektroniki wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwenye viwanja vya Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.

PMO_1341

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ngao ya shukurani kutoka  kwa Mwenyekiti  wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dkt. Ludigija Boniface Bulamile baada ya kufungua semina Endelevu ya 29 ya Bodi hiyo  kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018

PMO_1392

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na viongozi walioshiriki katika Semina Endelevu ya 29 ya Bodi ya Usajili  wa  Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi baada ya kufungua semina hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018. Kutoka kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi  na Mawasiliano, Profesa, Makame Mbarawa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi, Joseph Nyamhanga na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dkt. Ludigija Boniface Butamile.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

………………

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wabunifu majengo na wakadiriaji majenziwajiepushe na vitendo vya rushwa ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inalingana na thamani ya fedha inayotumika.

 

’’Epukeni vitendo vya rushwa ambavyo huisababishia Serikali hasara kubwa na kuleta usumbufu kwa wananchi.Ni matumaini yangu kuwa mtafanya kazi kwa weledi na kufuata maadili ya taaluma zenu’’. 

 

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Mei 18, 2018) wakati akifungua semina endelevu ya 29 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, iliyofanyika Jijini Dodoma.

 

Amesema wataalamu hao ni vema wakahakikisha majengo wanayobuni yanakuwa bora katika muonekano na mandhari yake iwe yenye kuvutia na yenye kuzingatia utunzaji wa mazingira na matumizi bora na endelevu ya nishati.

 

Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzikwa kuchagua mada inayohusu jukumu la wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi katika kuendeleza viwanda hapa nchini.

 

Amesema anatambua kuwa ujenzi wa viwanda unaendana na ujenzi wa miundombinu kama majengo, barabara, madaraja, miundombinu ya nishati na viwanja vya ndege, ambayo ni muhimu katika kuimarisha uchumi wa viwanda. 

 

’’Hivyo, wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi mna mchango mkubwa sana katika kufikia uchumi wa viwanda. Nitoe rai kwa Bodi ihakikishe kuwa miradi yote ya majengo pamoja na miundombinu mingine inashirikisha wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi katika ubunifu na usimamizi wa ujenzi wake.’’

 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amezitakataasisi za Serikali na waendelezaji binafsi wahakikishe wanatunza majengo ya kale, kama Sheria ya Mambo ya Kale inavyoelekeza.

Amesema nchi nyingi duniani zinaenzi majengo ya kale, ambayo yanatoa taswira ya nchi husika, ambapo kasi ya ukuaji wa sekta ya ujenzi hapa nchini haiwezi kuondoa dhana hiyo. 

 

’’Kwa msingi huo, napenda kusisitiza kuwa taasisi za Serikali na waendelezaji binafsi, wote wanapaswa kutunza majengo ya kale, kama Sheria ya Mambo ya Kale inavyoelekeza’’. 

 

Waziri Mkuu amesema jambo la muhimu ni kutoa elimu, ili wananchi waelewe umuhimu wa kutunza historia ya nchi yao kwa kupitia majengo ya kale ambayo pia yanaweza kuwa chanzo cha mapato kwa Serikali kupitia sekta ya utalii.

 

About Alex

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × 5 =