Wednesday , January 16 2019

Home / BIASHARA / WANAHISA CRDB WATAKIWA KUNUNUA HISA KWA WINGI

WANAHISA CRDB WATAKIWA KUNUNUA HISA KWA WINGI


PICHANI: Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akizungumza kwenye semina ya Wanahisa wa benki hiyo. Semina hiyo imefanyika leo Mei 18, 2018 kwenye Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha ikiwa ni utangulizi wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB kesho Mei 19, 2018. (Picha Zote na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).

Mtoa mada kwenye semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB Dkt. Blandina Kilama iliyofanyika leo Mei 18, 2018 Ukumbi wa AICC jijini Arusha. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).

Wanahisa wa Benki ya CRDB wakisikiliza watoa mada (hawapo pichani) kwenye semina iliyofanyika leo Mei 18, 2018 kwenye Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha, ikiwa ni utangulizi wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB kesho Mei 19, 2018. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).


Mtoa mada kwenye semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB Grace Joachim. Semina hiyo imefanyika leo Mei 18, 2018 kwenye Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha ikiwa ni utangulizi wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB kesho Mei 19, 2018. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).

Na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog. Arusha

WANAHISA wa Benki ya CRDB wameshauriwa kununua hisa kwa wingi ili kuweza kujiletea maendeleo, kwani ununuaji wa hisa hasa wakati kampuni husika imepata mgogoro wa muda mfupi bei yake inashuka.

Hayo yalisemwa leo Mei 18, 2018 na mtoa mada Dkt. Blandina Kilama kwenye Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) jijini Arusha.

Dkt. Kilama alisema wanahisa hao wanatakiwa kununua hisa bei zikiwa ndogo na kuuza hisa hizo bei ikiwa kubwa, lakini pia wanatakiwa kununua hisa muda mfupi kabla ya gawio, kwani uhitaji wa hisa hupanda.

“Nunua hisa bei inapokuwa ndogo, uza hisa bei inapokuwa kubwa. Uza hisa kabla ya gawio, kwani uhitaji wa hisa husika hupanda. Na pia nunua hisa muda baada ya dirisha la gawio kufungwa, uhitaji wa hisa husika hushuka. Pia nunua wakati kampuni imepata mgogoro au changamoto ya muda mfupi, kwani bei hushuka, na nunua hisa iwapo thamani inapanda

“Tunawekeza tukiwa na matarajio ya kupata faida katika uwekezaji wetu. Hili laweza kuwa lengo la muda mfupi au mrefu. Changanya hisa za muda mfupi na mrefu, kampuni ambayo inatoa gawio ama ongezeko la thamani, changanya hisa za huduma na viwanda, mfano usafiri na kuchakata vyakula, changanya makampuni mapya na makongwe, kampuni yenye kukua kama ya nishati ama kampuni ambayo imekuwepo muda mrefu” alisema Dkt. Kilama.

Dkt. Kilama amesema watu wengi hawana mpango mkakati wa kimaendeleo, na wenye mkakati huo hawajauandika, hivyo ili mtu kuendelea anahitaji kuweka mkakati ulioandikwa, utamuwezesha kuwa na kumbukumbu, lakini pia kumuwezesha kufanikiwa.

“Tengeneza mpango mkakati binafsi na uutathmini kila wakati. Katika kutekeleza mpango wako wa mwaka, tenga fedha za kutosha kwa ajili ya hisa kila mwezi. Pia katika kutekeleza mpango wako wa kila mwaka, tenga muda wa kutosha kwa ajili ya kutathmini hisa kila mwezi” alisema Dkt. Kilama.

Dkt. Kilama amewataka wanahisa hao kutumia Soko la Hisa kama njia ya kujiongezea mtaji wa awali, kutekeleza maamuzi yako na kuyasimamia na kuona mtu anafanikiwa. Kesho Mei 19, 2018, Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa CRDB ndiyo utafanyika, ambapo mambo mbalimbali ya benki hiyo yatazungumziwa.

About Alex

Check Also

PICHA 1

TRA YAKUSANYA TRILIONI 7.9 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 6 YA MWAKA WA FEDHA 2018/19

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

9 + four =