Wednesday , January 16 2019

Home / MICHEZO / SIMBA WALAMBA SH.MILIONI 100 KUTOKA SPORTPESA KWA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU

SIMBA WALAMBA SH.MILIONI 100 KUTOKA SPORTPESA KWA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas akizungumza jambo kabla ya makabidhiano ya hundi hiyo kufanyika.

Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa, Pavel Slavkov, (kushoto) akiwakabidhi hundi ya Sh. milioni 100, viongozi wa Simba na Nahodha wao John Bocco.

Kaimu Makamu wa Rais wa Simba Iddi Kajuna, akitoa neno la shukurani.

Baadhi ya wachezaji wa Simba na makocha wa timu hiyo wakiwa ndani ya Ofisi za SportPesa.

Wachezaji na viongiozi wa Simba na SportPesa wakiwa katika picha ya pamoja.

Habari/Picha:Musa Mateja\GPL.

…………..

KLABU ya Simba leo imekabidhiwa kitita cha Sh. milioni 100 kutoka kampuni ya SportPesa Ltd ikiwa moja ya fedha walizoahidiwa na kampuni  hiyo wakichukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mujibu  wamkataba walioingia nayo kama wadhamini wao wakuu.

Hafla ya makabidhiano ya kitita hicho imefanyika kwenye ofisi za SportPesa zilizopo maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam huku ikihudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili sambamba na wachezaji wa Simba wakiongozwa na nahodha wao John Bocco ambaye alifanya zoezi la kukabidhi kombe kwa wadhamini hao.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Iddi  Kajuna, alisema kuwa: “Tunaishukuru sana SportPesa kwa kututia nguvu tangu mwanzo wa Ligi hadi leo  hii ambapo wametukabidhi hundi hiyo ya shilingi milioni 100, bila kujali hata kuwa bado tuna mchezo mmoja ili tukamilishe ratiba yetu.

“Pia tunawashukuru SportPesa kwa kutuwezesha kulipa mishahara ya wachezaji wetu mapema, jambo ambalo tunaamini kwa namna moja au nyingine limechangia kwa kiasi kikubwa kwetu kuibuka mabingwa wa Tanzania kwani bila kutoa mishahara kwa wakati yawezekana  leo hii tusingeweza kufikia malengo yetu,” alisema Kajuna.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema: “Kwa niaba ya kampuni yetu ya SportPesa nawapongeza sana Simba kwa kuwatendea haki mashabiki wa Simba kwani kufanya hivyo mmetupa heshima kubwa sana sisi wadhamini wenu wakuu, kwani mmeitendea haki sana nembo yetu kiasi cha kampuni yetu kuamini kuwa imefanya jambo muhimu kuwa wadhamini wenu wakuu,” alisema Abbas.

About Alex

Check Also

IMG_5775

Wananchi kata ya Kala Wamlilia RC Baada ya kukosa Mawasiliano ya Simu Una Radio

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akiongea na wananchi wa Kijiji cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 − six =