Sunday , October 21 2018

Home / MICHEZO / YANGA VS AZAM FC KUMALIZA LIGI USIKU UWANJA WA TAIFA JUMATATU

YANGA VS AZAM FC KUMALIZA LIGI USIKU UWANJA WA TAIFA JUMATATU

20180524_210635-640x361

Mchezo wa mwisho wa Yanga katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utachezwa saa 2:00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Mei 28, mwaka huu.

Taarifa ya Bodi ya Ligi iliyotolewa na Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura, imesema Yanga na Azam zitacheza saa 2:00 usiku ili kutoa nafasi kwa Kituo cha Televisheni cha Azam TV chenye haki za kurusha Mbashara VPL, wakati michezo mingine yote itaanza saa 10:00 jioni.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kwani Azam na Yanga zipo katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya pili katika ligi huku ubingwa ukiwa tayari umechukuliwa na Simba yenye pointi 68.
.
Kwa sasa Azam ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 55 huku Yanga yenye mchezo mmoja mkononi ikiwa nafasi ya tatu na pointi 51.

About Alex

Check Also

5105576-6283433-He_then_scored_what_proved_to_be_the_winning_goal_of_the_match_f-m-61_1539723772722

UFARANSA YAITANDIKA UJERUMANI 2-1 MECHI YA LIGI YA MATAIFA YA ULAYA

    Antoine Griezmann akiinua mkono juu kushangilia kishujaa baada ya kuifungia mabao yote mawili …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

20 − five =