Tuesday , March 26 2019

Home / MCHANGANYIKO / MTENDAJI MKUU TEMESA AFUNGUA MAFUNZO YA VIONGOZI TEMESA

MTENDAJI MKUU TEMESA AFUNGUA MAFUNZO YA VIONGOZI TEMESA

PIC 1

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu katikati akisisitiza jambo wakati alipokua akizungumza na uongozi wa wakala huo (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Uongozi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) katika ukumbi wa mikutano Bohari Kuu ya Dawa(MSD) Keko jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa wakala huo CPA. Hans Lyimo na kushoto ni mkufunzi wa mafunzo hayo Bi. Zuhura Sinare Muro.

PIC 2

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu katikati akifurahia jambo wakati alipokua akizungumza na uongozi wa wakala huo (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Uongozi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) katika ukumbi wa mikutano Bohari Kuu ya Dawa(MSD) Keko jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa wakala huo CPA. Hans Lyimo na kushoto ni mkufunzi wa mafunzo hayo Bi. Zuhura Sinare Muro.

PIC 3

Sehemu ya Viongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA wanaohudhuria mafunzo kwa viongozi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) katika ukumbi wa mikutano Bohari Kuu ya Dawa(MSD) Keko jijini Dar es Salaam wakimsikiliza mkufunzi wa mafunzo hayo Bi. Zuhura Sinare Muro aliyesimama katikati.

PIC 4

Sehemu ya Viongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA wanaohudhuria mafunzo kwa viongozi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) katika ukumbi wa mikutano Bohari Kuu ya Dawa(MSD) Keko jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Dkt Mussa Mgwatu (hayupo pichani) alipokua akifungua mafunzo hayo mapema leo.

PIC 5

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu katikati (mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wakala huo wanaohudhuria mafunzo kwa viongozi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) katika ukumbi wa mikutano Bohari Kuu ya Dawa(MSD) Keko jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) Bi. Zuhura Sinare Muro.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA

……………

Na Alfred Mgweno TEMESA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu ameutaka uongozi wa wakala huo kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi ili kupata matokeo bora na kuongeza tija katika wakala.

Dkt. Mussa Mgwatu ameyasema hayo leo wakati akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa wakala huo yanayofanyika katika Ukumbi wa mikutano Bohari Kuu ya Madawa (MSD) Keko jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi kimkakati na kwa wakati maalumu huku yakilenga zaidi masuala ya Akili Hisia, Uongozi Binafsi pamoja na kujitambua kama kiongozi.

‘’Furaha yangu kuhusu matayarisho ya siku ya leo yatakuwa ni mafunzo muhimu sana kwetu kwasababu naweza nikawa nikiwalaumu viongozi wangu kumbe siwawezeshi kufanya vizuri, nina uhakika mafunzo haya yatawawezesha kupata viongozi walio bora sio tu kwa TEMESA au Taifa bali viongozi wa Afrika na Dunia kwa ujumla’’, alisema Dkt. Mgwatu. Aliwahimiza pia viongozi wanaopatiwa mafunzo hayo kuyatumia vizuri ili kuhakikisha wanaporudi wanafanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu mkubwa.

Naye mratibu wa mafunzo hayo kutoka Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) Bi. Zuhura Sinare Muro aliwataka viongozi hao kuyazingatia mafunzo hayo na kuyapa kipaumbele kwani yatasaidia kuwaweka viongozi hao vizuri kimaadili na pia kuwaongezea tija na uzoefu katika utendaji wao. Bi Sinare aliushukuru pia uongozi wa TEMESA kwa kuwaamini na kukubali kupewa mafunzo hayo na Taaasisi hiyo.

Mafunzo hayo yatakayochukua siku nne yanatarajiwa kumalizika ifikapo ijumaa ya Tarehe 8 Mwezi wa Juni mwaka huu.

About Alex

Check Also

AA

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fifteen − five =