Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / RC MAKONDA KUWASHIKISHA ADABU WACHAFUZI WA MAZINGIRA.

RC MAKONDA KUWASHIKISHA ADABU WACHAFUZI WA MAZINGIRA.

KON1

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametangaza kuanza kwa oparesheni kabambe ya kuwakamata na kuwatoza faini wachafuzi wa Mazingira kuanzia July Mosi kwa lengo la kuhakikisha jiji linakuwa kwenye Hali ya usafi kama majiji mengine ulimwenguni.

RC Makonda amesema ameandaa vijana zaidi ya 4,000 kutoka Jeshi la kujenga Taifa JKT ambao watafanya kazi ya kuwakamata watupaji wa taka barabarani na mitaani.

Vijana hao 4,000 ni wale waliomaliza mafunzo ya JKT na hawana kazi ambapo RC Makonda ameamua kuwachukuwa kwaajili ya kufanya kazi hiyo na kwenye kiasi cha faini watakazo watoza wachafuzi wa mazingira 40% itaenda kwa vijana hao na 60% itaingizwa serikalini.

Aidha RC Makonda amesema hawezi kukubali kuona jiji linakuwa kwenye hali ya uchafu wakati ipo sheria ya mwaka 2004 inayotoa mamlaka ya kuwawajibisha wananchi wenye tabia kuchafua mazingira kwa makusudi.

Itakumbukwa kila mwaka viongozi wamekuwa wakihimiza usafi na hata alipokuja Rais Barack Obama miaka kadhaa iliyopita barabara zilipigwa deki na alipoondoka uchafu ukaendelea na hivi karibuni Rais Magufuli alifanya usafi Kama sehemu ya kuhimiza usafi lakini bado watu wamekaidi, pia ulianzishwa utaratibu wa usafi kila jumamosi watu wasifungue maduka hadi wafanye usafi lakini bado pia wamekaidi jambo ambalo RC Makonda ameamua sasa kuja na mkakati wa kuwatumia vijana wa JKT wasiokuwa na kazi  kufanya jukumu la kuwakamata wachafuzi wa mazingira.

KON2

About bukuku

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

15 − 4 =