Thursday , February 21 2019

Home / MICHEZO / AZAM FC YAIPA PIGO LA TATU SINGIDA UNITED

AZAM FC YAIPA PIGO LA TATU SINGIDA UNITED

 

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Azam FC imefanikiwa kumrejesha kiungo wake, Mudathir Yahya kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili kutoka Singida United.
Mudathir, kiungo Mzanzibar hodari leo amesaini mkataba huo mbele ya Makamu Mwenyekiti, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na Meneja Philipo Alando.
Mudathir alikwenda Singida United msimu uliopita baada ya kumaliza mkataba wake Azam na baada ya kazi nzuri akiwa na timu hiyo ya Uwanja wa Namfua amerejeshwa nyumbani.
Ikumbukwe mchezaji huyo aliibuliwa katika mfumo wa soka ya vijana ya klabu hiyo, maarufu kama Azam Akademi mwaka 2013, kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza – ingawa baadaye ushindani wa namba ukamsukumia nje.

Screenshot_20180613-150242-570x400
Mudathir Yahya (kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ baada ya kusaini leo
 
Screenshot_20180613-150154
Mudathir Yahya akisani mkataba wa kurejea Azam FC. Kushoto ni Meneja Philipo Alando

Mudathir anakuwa mchezaji wa pili kusaini Azam FC kutoka Singida United ndani ya wiki mbili, baada ya Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu na kwa ujumla ni mtu wa tatu kutoka Namfua kuhamia Chamazi, baada ya kocha Mholanzi pia, Hans van der Pluijm.
Azam pia imewasajili Mzimbabwe mwingine, Donald Ngoma kutoka Yanga SC na mzawa, mshambuliaji Ditram Nchimbi.

About Alex

Check Also

Yangarahapic

YANGA SC YAVUNJA MWIKO CCM KIRUMBA MWANZA, YAICHAPA 2-1 MBAO FC

Na Mwandishi Wetu, MWANZA YANGA SC imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Mbao FC …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 3 =