Sunday , August 19 2018

Home / MCHANGANYIKO / VIDEO:DKT. NDUGULILE AAGIZA MADAKTARI KUCHUNGUZA UKATILI KWA WATOTO WACHANGA

VIDEO:DKT. NDUGULILE AAGIZA MADAKTARI KUCHUNGUZA UKATILI KWA WATOTO WACHANGA

Pix 1

 

Watoto wa Mkoa wa Arusha wakiwa katika Maandamano ya Siku ya Mtoto wa Afrika yenye Kauli Mbiu isemayo Kuelekea uchumi wa Viwanda Tusimuache Mtoto Nyuma.

Pix 2

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na watoto waliokusanyika katika kiwanja cha mpira cha Shekh Amri Abed Jijini Arusha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika

Pix 3

Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Sihaba Nkinga akielezea chimbuko la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Jijini Arusha .

Pix 4

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kamati ya ulinzi na usalama kwa wanawake na watoto mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Jijini Arusha.

Pix 5

Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Sihaba Nkinga akisalimiana na  Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la CWDC linalojishughulisha na kupambana na ukatili kwa wanawake na watoto Bi.Hindu Mbweso mara baada ya kuvalishwa vazi la kimasai ikiwa zawadi kutoka kwa watoto wa kimasai ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wake katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

…………………

NA ANTHONY ISHENGOMA WAMJW ARUSHA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ameagiza wataalamu wa Afya wanapofanya uchunguzi kwa watoto waaangalie pia kama wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa  ukeketaji.

Amesema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika leo jijini Arusha na kuongeza kuwa baada ya Ngariba kuzuiwa kufanya ukeketaji kwa vijana wa kike sasa wamebadilisha mbinu zao na kuanza kukeketa vichanga.

Amesema matukio ya ukatili wa jinsia ni mengi kuliko matukio ya ujambazi hapa nchini ndio maana Serikali  imeanzisha madawati 500 ya Jinsia kwa Jeshi la polisi kote nchini pamoja na kuanzisha namba mpya simu ya 116 ambapo mtu yoyote ambaye amefanyiwa ukatili wa kijinsia anaweza kuitumia kupata msaada.

Amesema serikali pia imeanzisha madawati ya kamati ya ulinzi na usalama kwa wanawake na watoto katika ngazi ya Mkoa hadi Wilaya kwa lengo la kuhakikisha haki zote za Msingi kwa watoto zinalindwa na kutekelezeka ili watoto watanzania waweze kushiriki kikamilifu katika Tanzania ya viwanda.

Pia Naibu Waziri huyo ametumia sehemu ya maadhimisho haya kuzindua kamati ya ulinzi na usalama kwa wanawake na watoto mkoani Arusha na kuwakabidhi Mwongozo uliondaliwa na Wizara  kama nyenzo ya kufanyia kazi kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Wakati huo huo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bi. Sihaba Nkinga katika hotuba yake kumkaribisha Mgeni rasmi amesema maadhimisho ya mtoto wa Afrika yanatoa nafasi kwetu sisi watanzania kutafakari na kujitathimini ni namna gani tunatekeleza kwa vitendo haki za Msingi za watoto.

Bi. Sihaba amesema kuwa Maadhimisho haya kimsingi yanaadhimishwa Kitaifa kila baada ya miaka mitano lakini pia huadhimishwa kila mwaka katika ngazi ya Mkoa na Wizara huadhimisha kwa kushirikiana na mkoa kwa kuzingatia agenda iliyopo hivyo Arusha inaongoza kwa mikoa mitano yenye ukatili mkubwa kwenye eneo la ukeketaji.

Amezitaja haki za watoto kuwa ni haki ya kusikilizwa, kuendelezwa, kuishi, kulindwa na kutobaguliwa lakini pia amesema kuna ukatili wa aina nyingi  akiutaja Mkoa Arusha wa Arusha kuongoza kwa vitendo vya ukeketaji.

Maadhimisho haya yanafanyika kufuatia mauaji ya watoto zaidi ya 2,000 yaliyofanyika katika kitongaji cha SOWETO Nchini Afrika ya Kusini mwaka 1976 yaliyosababishwa na Polisi wa Serikali ya Makaburu ya wakati huo walio kuwa wanaandamana kupinga mfumo wa utoaji elimu wa kibaguzi uliokuwa unawakandamiza watoto wa kiafrika.

 

About Alex

Check Also

DSC_1656

MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA KISASA NYAMANZI VISIWANI ZANZIBAR WAZINDULIWA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata Utepe kuashiria …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × four =