Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / Mafunzo ya Mfumo Mpya wa Malipo (Epicor 10.2) kwa Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara Yaendelea Jijini Dodoma

Mafunzo ya Mfumo Mpya wa Malipo (Epicor 10.2) kwa Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara Yaendelea Jijini Dodoma

Pix 1

Mweka Hazina wa Jiji la Arusha, Bw. Mbwana Msangi (katika) akifanya mazoezi ya kutumia mfumo wa malipo epicor 10.2 pamoja na Wahasibu wa Jiji hilo Bw. Juma Manyika (kulia) na Bi. Fadhila Shemte (kushoto) jana Jijini Dodoma.

Pix 2

Mkufunzi wa mafuzo ya mfumo wa malipo epicor 10.2 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Augustino Manda akitoa maelekezo ya namna ya kutumia mfumo mpya wa epicor 10.2 Wahasibu wa Halmashauri ya Arusha, jana Jijini Dodoma.

Pix 3

Mkufunzi wa mafuzo ya mfumo wa malipo epicor 10.2 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Augustino Manda (aliyesimama) akiwajengea uwezo Waweka Hazina na Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara namna ya kutumia mfumo huo unaotarajia kuanza kutumika Julai 1, mwaka huu na Halmashauri zote nchini.

Pix 4

Wahasibu kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha na Itigi wakifanya mazoezi ya kutumia mfumo mpya wa malipo epicor 10.2 wakati wa mafunzo ya mfumo huo Jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanaratibiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

Pix 5

Waweka Hazina na Wahasibu kutoka Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara wakifutilia mafunzo ya mfumo wa epicor 10.2 yanayoendelea Jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanatolewa katika vituo Sita nchini ambavyo ni Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza, Kagera na Mtwara yakihusisha Waweka Hazina, Wahasibu, Maafisa Manunuzi, Wakaguzi wa Ndani na Maafisa TEHEMA lengo likiwa ni kuwajengea uwezo watumiaji wa mfumo huo namna ya kutumia mfumo huo unaotarajia kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini.

(Picha Na. Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma)

 

About Alex

Check Also

3

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 30

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza na wajumbe wa kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 − 4 =