Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO TAREHE 13 JUNI 2018

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO TAREHE 13 JUNI 2018

B0a

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo wakati wa kuchangia hoja ya iliyowasiliwashwa na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa George Boniphace Simbachawene(hayupo pichani) kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Dodoma wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma. Simbachawene amewasilisha hoja ya kuazimia Bunge litoe pongezi ikwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kuupa hadhi mji wa Dodoma kuwa Jiji.

B0b

Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa George Boniphace Simbachawene akiwasilisha hoja kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Dodoma ya kuazimia Bunge litoe pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kuupa hadhi mji wa Dodoma kuwa Jiji wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma. Bunge limepitisha azimio hilo kwa pamoja na kuazimia kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake huo wa kuupa hadhi mji wa Dodoma.

B0c

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Selemani Jafo akifafanua jambo wakati wa kuchangia hoja ya iliyowasiliwashwa na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa George Boniphace Simbachawene (hayupo pichani) kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Dodoma wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma.Simbachawene amewasilisha hoja ya kuazimia Bunge litoe pongezi ikwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kuupa hadhi mji wa Dodoma kuwa Jiji.

B1

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma.

B2a

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mtamaa Nape Moses Nnauye wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma.

B2b

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa(kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma.

B3

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma.

B4

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge wanawake na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mama Gaudensia Kabaka (mwenye mvi kichwani) walipotembelea Bungeni wakati wa Mkutano wa 11 wa Bunge, kikao cha Hamsini leo tarehe 13 Juni, 2018 Jijini Dodoma.

Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma

About Alex

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

seven + 6 =