Wednesday , January 16 2019

Home / MCHANGANYIKO / NAIBU WAZIRI WA ELIMU OLE NASHA: SERIKALI HAITAFUMBIA MACHO VITENDO VYA UDHALILISHAJI DHIDI YA WANAFUNZI

NAIBU WAZIRI WA ELIMU OLE NASHA: SERIKALI HAITAFUMBIA MACHO VITENDO VYA UDHALILISHAJI DHIDI YA WANAFUNZI

Naibu Waziri  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha amesema  Serikali haitafumbia macho vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanafunzi na kuwa Sheria kali zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa kauli hiyo Leo mkoani Dodoma wakati wa mahojiano Maalumu na Shirika la Utabgazaji la Taifa – TBC ambapo amesema Sheria za nchi ziko wazi kwa mtu yeyote atakaebainika kufanya vitendo vya ngoni basi adhabu yake ni miaka 15 jela hadi kifungo Cha maisha.

Mheshimiwa Ole Nasha pia ameitaka idara ya Uthibiti ubora nchini kuhakikisha unafanya ufuatiliaji kwa lengo la kuhakikisha Elimu bora inapatikana nchini kwa kuwa hilo ndiyo jukumu Lao.

“ Kuna maeneo bado Idara ya uthibiti ubora haijafanya vizuri, mfano katika hili tukio la st. florence Idara hiyo ina kitu cha kujibu,” licha ya kuwa vyombo vingine vya Sheria vinaendelea na uchunguzi lakini na sisi ndani  ya Wizara tunafanya uchunguzi kuona nani  kazembea katika suala hilo,”alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.

Naibu Waziri pia amewataka wazazi Kuhakikisha watoto wote waliofika umri wa kwenda shule wanakwenda shule kwa kuwa hivi sasa  Elimu msingi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato Cha Nne inatolewa bure.

Akizungumzia kuhusu viwanda Mheshimiwa Ole Nasha amesema vyuo vya ufundi ndiyo njia sahihi ya kulipeleka Taifa katika UChumi wa Kati, hivyo kupitia vyuo hivyo Taifa litapata  nguvukazi na   sahihi ambayo itatumika kwenye viwanda.

About Alex

Check Also

5a-min

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × three =