Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / RC MAKONDA AANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

RC MAKONDA AANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

IMG-20180613-WA0101
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameanza kufanyia kazi agizo la Rais Dr. John Magufuli la kufuatilia taratibu za ujenzi wa Barabara ya kutokea Makao Makuu ya BAKWATA hadi Biafra na tatizo la mfumo wa maji kwenye eneo la Kinondoni Shamba. 
Mapema leo RC Makonda amefanya ziara ya ukaguzi na kubaini nyumba nyingi kwenye eneo hilo zimejengwa kwenye hifadhi ya barabara na baadhi ya watu tayari wamelipwa fidia ambapo amewataka wananchi kushirikiana na TARURA kuhakikisha ujenzi wa barabara unaanza Mara moja.
IMG-20180613-WA0096
Aidha RC Makonda ameagiza TANESCO, DAWASCO na TTCL kushirikiana kwa karibu na TARURA kuondoa miundombinu yao ili kasi ya ujenzi uanze. 
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Kinondoni Bwana Leopold Runji amesema tayari wameanza utekelezaji wa maagizo waliyopatiwa na watahakikisha ujenzi unaenda kwa kasi na kukamilika kwa wakati.
IMG-20180613-WA0097
Itakumbukwa siku ya Jana June 12 Rais Dr. John Magufuli alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti na maendeleo ya ujenzi wa Makao Makuu ya BAKWATA ambapo wakati wa kuondoka alipata wasaha wa kuzungumza na Wananchi ambao waliwasilisha kwake ombi la ujenzi wa Barabara.

About Alex

Check Also

IMG_7568

Lishe Endelevu kumaliza Tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twelve + 7 =