Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / KIPANDE CHA RELI YA KATI KUANZIA DAR ES SALAAM HADI ISAKA (KM 970) KUFANYIWA UKARABATI MKUBWA

KIPANDE CHA RELI YA KATI KUANZIA DAR ES SALAAM HADI ISAKA (KM 970) KUFANYIWA UKARABATI MKUBWA

index

Mtaalam wa Mambo ya Jamii Catherine Mroso akitoa elimu ya mradi wa uboreshaji wa reli ya katiDar es salaam -Isakakwa wanakijiji wa Kwara, Katika Halmashauri ya wilaya ya Kibaha vijijini.

8 7

Wanakijiji wa Halmashauri ya kibaha vijijini, wakifuatilia kwamakini maelelezo yanayotolewa katika mkutano unaoendeshwa na wataalamu kutoka shirika la reli Tanzania – TRC Kuhusu uboreshaji wa Reli ya kati Dares salaam- Isaka

…………………

SHIRIKA LA RELI TANZANIA – TRC

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: MRADI WA UBORESHAJI WA RELI YA KATI

Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Uongozi wa TRC wamedhamiria kukarabati reli ya kati kipande cha kuanzia  Dar es Salaam – Isaka (km970). Mradi huu umefadhiliwa na Benki ya dunia na kutekelezwa na Shirika la Reli Tanzania katika kipindi cha muda wa miaka miwili kuanzia juni 2018 hadi juni 2020.

Lengo la uboreshaji wa reli ya kati ni kutoa usafiri wa kuaminika na kukuza upatikanaji wa huduma bora Nchini. Na maboresho hayo yatasaidia kuinua uwezo wa kubeba mzigo toka chini ya tani 13.5 za uzito wa eskeli hadi tani 18.5 kwa kufanya yafuatayo:

  1. Kutandika upya njia za reli zenye uzani wa paundi 80 kwa urefu wa kilometa 312
  2. Kufanya ukarabati wa njia ya reli iliyosalia kwa urefu wa kilometa 658
  3. Kufanyia ukarabati makaravati  na madaraja 442
  4. Kuboresha mfumo wa mawasiliano
  5. Kuboresha vituo vya kupakia na kupakua mizigo vya bandari ya Dar es Salaam, ilala na Bandari kavu ya Isaka.
  6. Ununuzi wa vichwa vitatu vya treni (vipya) na mabehewa mapya 44 ya mizigo

Katika kufikia malengo haya TRC itaingia mikataba 64 kati ya hiyo 32 ni ya kuajiri Washauri mbalimbali, 6 ni ya ujenzi na 24 ununuzi wa vifaa mballimbali na mikataba miwili ni ya huduma. Mpaka sasa zaidi ya 50% ya mikataba hii imeshasainiwa.

Kupitia Mradi huu TRC pia imetengeneza mpango endelevu wa matengenezo ya miundombinu ili kufanya njia ya usafiri huu kuwa wa uhakika  na kuaminika. Kuimarika kwa usafiri wa reli kutapunguza gharama za matengenezo ya barabara na hivyo serikali kuelekeza bajeti iliyookolewa  kwenda kwenye huduma nyingine za kijamii.

Maendeleo ya utekelezaji wa Mradi

Kabla ya kuanza rasmi ukarabati wa njia za reli mwezi juni, TRC inaendelea kufanya kampeni ya uhamasishaji  katika Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, katika Manispaa ya Ilala na Halmashauri ya Kibaha vijijini, ili kujenga uelewa kwa wananchi kuhusiana Mradi huu kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara katika kata na vijiji vinavyopitiwa na mradi huu.

Kampeni hiyo ya uhamasishaji inaambatana na kuelezea faida za mradi wakati wa ujenzi ambazo ni kuwepo kwa fursa za ajira, kukua kwa kipato cha wananchi maeneo ya mradi na kujengewa ujuzi kwa wote watakaoshiriki kwenye shughuli za ujenzi.

Pia wananchi wamepata fursa ya uelewa faida za mradi baada ya uboreshaji wa reli ya kati ambazo ni kuboresha na kuongeza kiwango cha ubebaji mizigo kwa miuondo mbinu ya reli na madaraja. Kuongezeka kwa mwendokasi wa treni kutoka kilometa 35 kwa saa hadi kufikia kilometa 70 kwa saa na hivyo kupunguza gharama na muda wa usafirishaji mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi bandari kavu ya Isaka hadi kufikia saa 24 kutoka zaidi ya masaa 36 ya sasa.

Kampeni ya uhamasisha kwa wananchi imepelekea wapate kutambua hatua za uboreshaji ambapo Mradi huu umegawanyika katika vipande viwili, kipande cha kwanza kitaanzia Dar es Salaam  hadi kilosa (kilometa 283), kipande cha pili ni kilosa hadi Isaka (kilometa 687) na vipande hivi vimeshapata wakandarasi na ujenzi unataraji kuanza mapema juni 2018.

Kampeni ya uhamasishaji ni enedelevu mpaka pale mradi utakapokamilika, Uongozi wa TRC umesisitiza mambo ya kuzingatia kwa wananchi ambao reli ya kati inapita katika maeneo wanayoishi, ambayo ni: Hairuhusiwi shughuli zozote za kibinadamu katika maeneo ya reli ikiwa ni pamoja na biashara,kilimo na ufugaji.

Wafanyabiashara wote watapaswa kupata kibali maalum cha biashara kutoka katika stesheni.Wakulima na wafugaji hawaruhusiwi kabisa kufanya shughuli za kilimo na ufugaji katika eneo la reli,vilevele wafugaji wanapaswa kutumia vivuko vya mifugo vinavyotambulika na kuepuka kuvusha mifugo yao maeneo yasiyo na vivuko.

Tahadhari, Jamii inapaswa kuchukua tahadhari za kiafya na tabia zozote hatarishi ili kuepuka maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kaswende,kisonono na hata maambukizi ya  virusi vya UKIMWI.

 

About Alex

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

20 + twelve =