Thursday , March 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / WAZIRI UMMY AZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUWEKA KAMBI ZA UCHANGIAJI DAMU MARA TATU KWA MWAKA

WAZIRI UMMY AZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUWEKA KAMBI ZA UCHANGIAJI DAMU MARA TATU KWA MWAKA

IMG-20180613-WA0039

Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati akitoa tamko la siku ya wachangiaji damu Duniani inayofanyika kila mwaka tarehe 14 Juni,ambapo mwaka huu itafanyika JIjini Dodoma

IMG_9702

.Meneja Mpango wa Damu Salama SDkt.Magdalena Lyimo(wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu shughuli nzima ya ukusanyaji wa damu nchini ambapo mwaka huu wamepanga kukusanya chupa 375,203 ukilinganisha na miaka ya nyuma.wa kwanza kushoto ni katibu wa chama cha wanawake wa tasnia ya filamu nchini ambao wanahamasisha uchangiaji damu nchini(davina)

IMG_9629

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini wakisikiliza tamko la waziri wa Afya mhe.Ummy Mwalimu

IMG_9672

kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Eliud Eliakim akiongea wakati wa tamko la maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu Duniani

IMG_9691

Waziri Ummy Mwalimu akitoa tamko la siku ya wachangiaji damu Duniani ambapo alisema wanufaika wakubwa wa damu hapa nchini ni wanawake wakati wa kujifungua na majeruhi wanaotokana na ajali za barabarani wakiemo bodaboda

PICHA NA WIZARA YA AFYA

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amezitaka halmashauri zote nchini kuweka kambi za uchangiaji damu mara tatu kwa Mwaka ili kuweza kufikia lengo la kukusanya damu kwa asilimia 60 kwa Mwaka.

Amesema hayo Leo wakati  wa kuelekea katika Maadhimisho ya Siku ya Uchangia Damu Duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika kesho,Asubuhi katika Jiji la Dodoma maeneo ya Nyerere Square na kuwaomba wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika Zoezi hilo ambalo ni muhimu kwa Taifa.

Amesema Matukio ya Uchangia damu yamekuwa yakiokoa maisha hasa kwa kina Mama pamoja na Watoto kwa hiyo ni wajibu wa kila Halmashauri kuratibu na kusimamaia zoezi hilo kwa utaratibu mzuri kwani hadi sasa Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha Asilimia 45 ya mahitaji ya damu.

Hata hivyo amesema kuwa kiwango cha Damu kinachohitajika kukusanya kwa mwaka kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani WHO ni asilimia moja ya idadi ya watu ambapo Tanzania inahitaji kukusanya chupa laki tano na arobaini ambayo bado haijafikiwa.

Pia Mhe.Mwalimu, amesema kuwa kwa sasa watajikita katika kukusanya damu za makundi adimu ambayo yamekuwa yakikosekana kwenye benki za damu kama kundi A negative,B negative, 0 negative na AB negative.

Kwa Upande wa Dk Magdalena Lyimo  ambaye ni meneja wa mpango wa damu salama amesema kuwa bado Tanzania haijafikia idadi ya chupa za damu zinazohitajika huku Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk.Nasoro Mzee  ameeleza kuwa kiasi cha damu kilichopo mkoa wa Dodoma bado ni kidogo hivyo Wadau wanahitajika kuhamasisha jamii ili iwe na utayari wa kuchangia damu bila wasiwasi

Siku ya uchangiaji damu duniani inaadhimishwa kila ifikapo 14 amapo Tanzania inategeea kuwatumia wasanii mbalimbali katika kuhamasisha uchangiai wa damu ili kuokoa maisha ya watanzania.

About Alex

Check Also

IMG_7568

Lishe Endelevu kumaliza Tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen − thirteen =