Thursday , January 17 2019

Home / MCHANGANYIKO / KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUWA KIPAUMBELE KATIKA KUCHOCHEA MAENDELEO

KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUWA KIPAUMBELE KATIKA KUCHOCHEA MAENDELEO

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MBUNGE wa
Ubungo, Saed Kubenea ametoa wito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha siasa na
badala yake kufanyakazi kwa kwaajili ya maendeleo.

Kubenea
ametoa kauli hiyo leo  jijini Dar es
Salaam alipotembelea miradi ya Maendeleo katika jimbo lake la Ubungo na
kuikabidhi.
Miradi
aliyoitembelea Kubenea ni wa ujenzi wa kibanda cha kupumzikia katika Zahanati
ya Mavurunza iliyopo Kimara ambao umegharimu sh. Milioni 7.7, miradi wa ujenzi
wa madarasa katika shule ya Msingi Mabibo ambao umegharimu Sh. milioni 17,
mradi wa kisima katika soko la Mabibo uliogharimu sh. Milioni 12 pamoja na
ujenzi wa ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kawawa.
Akizungumza
baada ya kutembelea na kuikabidhi miradi hiyo, Kubenea alisema ni vyema kufanya
kazi kwa kushirikiana na sio kuangalia chama.
“Mimi
sifanyi mambo haya kwaajili ya siasa, ninafanya kwaajili ya maendeleo ya
wananchi….ninajua hata siku nikiondoka itabaki historia kwamba Kubenea
alifanya kitu fulani.
“Kwahiyo
niwaombe viongozi wote, tusiangalie siasa eti huyu chama tawala, huyu
Chadema…tufanye kazi pamoja katika kuleta maendeleo ya Taifa letu,”
alisema Kubenea.
Kubenea
aliongeza kuwa maendeleo yana safari ndefu hivyo maeneo ya Hospitali, shule
yanahitaji kuboreshwa.
Akizungumzia
miradi hiyo Kubenea alisema fedha zake zimetoka katika mfuko wa jimbo ambapo ni
sehemu ya fedha za bajeti ya mwaka 2017/18.
Akitoa
shukrani kwa ujenzi wa Kibanda cha Mapumziko, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya
Mavurunza alisema walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya msongamano wa wagonjwa
ambao ulisababishwa na kutokuwa na sehemu ya kupumzika.
“Kwasasa
tunafanya kazi kwa uhuru na usiri kati ya mgonjwa na daktari….tunakushukuru
Mbunge wetu ambaye uliamua kujitolea fedha hizi kutoka katika mfuko wako,”
alisema Dorothy.
Aidha
Dorothy alisema Zahanati hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  jengo la wazazi kuhitaji ukarabati, kutokuwa
na uzio pamoja eneo hilo kuhitaji kusawazishwa ambapo Kubenea aliahidi
atalisawazisha kwa kipindi kifupi.
Naye Mkuu wa
Shule ya Mabibo, Hussein Mabibo alisema fedha zilizotolewa ambazo ni sh.
milioni 17 zimesaidia kujenga madarasa matano, kubadilisha vigae vilivyochakaa
na kuweka mabati, kupanga rangi shule, kukarabati ofisi ya walimu pamoja na
ofisi ya mwalimu Mkuu.
“Tunakuamini
wewe Mbunge wetu ukisema hua unatekeleza, hivyo tunaomba utusaidie pia
kukamilisha maktaba, ujenzi wa uzio wa shule kwaajili ya usalama wa wanafunzi
pamoja na ukarabati wa madarasa tisa ambayo yako katika hali mbaya,”
alisema Dady.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa na Soko la Mabibo, Yusuph Kilema alisema kisima
kilichojengwa katika soko hilo kimekamilika kwa asilimia 90 ambapo bado vitu
vichache ili kianze kutumika rasmi.

 Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi wa kata ya Mavurunza Kimara mara baada ya kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa katika zahanati ya Mavulunza lililojengwa na fedha za mfuko wa jimbo

 Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea  akiwa amembeba mmoja wa watoto waliofika kupata huduma katika Zahanati ya Mavurunza .

 Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akisoma gharama za ujenzi wa Mnara wa kupandisha maji juu katika kisima kilichojengwa katika soko la Mabibo Garment kwa fedha za mfuko wa jimbo

 Mhandisi wa maji wa Manispa ya Ubungo akitoa maelezo kwa Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea wakatia  alipotembelea miradi iijengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo.

 Mwalimu wa shule ya Msingi Mkwawa Mabibo akimueleza Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea kiasi cha fedha zinazohitajika katika umaliziaji wa ofisi za walimu.

 Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akiwa ameongozana na baadhi ya watendaji wa halmashauri na wafanyabishara wa soko la Mabibo

  Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akisalimiana na wananchi na Makada Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi.

  Mmoja ya wakazi wa Mavurunza akitoa pongezi kwa Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea mara bada ya kutekeleza ahadi zake kwa wakazi wa eneo hilo 

 wakazi wa Ubungo kata ya Mavurunza wakiwa wanasikiliza hotuba ya mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea 

 Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkwawa Mabibo

About Alex

Check Also

HA2

WAKULIMA KUSAJILIWA NA KUPATIWA VITAMBULISHO NCHINI

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akifungua  mkutano wa kitaifa wa wadau wa Tumbaku nchini leo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twenty + 12 =