Thursday , January 17 2019

Home / MICHEZO / SALAHA YUPO FITI ASILIMIA 100 KUWAVAA URUGUAY KESHO KOMBE LA DUNIA

SALAHA YUPO FITI ASILIMIA 100 KUWAVAA URUGUAY KESHO KOMBE LA DUNIA

 

Ripoti kutoka Urusi zinaeleza kuwa nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Misiri, Mohamed Salah ameshapona majeraha yake.

Mchezaji huyo anapewa nafasi kubwa ya kukiongoza kikosi cha Misri Ijumaa ya wiki ijayo dhidi ya Uruguay ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa taifa hilo katika michuano ya Kombe la Dunia inayoanza leo.

Salah aliumia katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa kuchezewa rafu na nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos kisha kusababisha kuondolewa nje ya Uwanja.

Kupona kwa Salah kumeongeza matumaini kwa Waafrika na Wamisri kwa ujumla kwenye safu ya ushambuliaji wa timu hiyo kutokana na mchango wake mkubwa Uwanjani.

About Alex

Check Also

74cd07906b28bc9b942b481f9f46f6ce

TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE

 Mkutano wa waandishi wote wa habari za michezo unatarajiwa kufanyika Jumapili Februari 10 mwaka huu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

10 + 19 =