Thursday , January 17 2019

Home / MCHANGANYIKO / Serikali Yawasilisha Bajeti Inayolenga Kuwainua Wananchi Kiuchumi

Serikali Yawasilisha Bajeti Inayolenga Kuwainua Wananchi Kiuchumi

B6

Baadhi ya Wabunge wakiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango na Naibu Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaji mara baada ya kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2018/19 leo tarehe 14 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

………………..

Na Jonas Kamaleki- MAELEZO, Dodoma.

Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amewasilisha makadrio ya bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 ambayo imelenga kumpunguzia mwananchi ugumu wa maisha na kuchochoea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Akishangaliwa na wabunge Dkt. Mpango amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi shupavu wa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ametaja mambo kadhaa ambayo yanonyesha uongozi mahiri wa Rais Magufuli kuwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya kisasa yenye viwango vya kimataifa (Standard Gauge), Kufufua Shirika la Ndege kwa kununua ndege saba zikiwemo mbili kubwa (Dreamliner) zenye uwezo wa kubeba abiria 262 kila moja, kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima na kuondoa watumishi hewa na wenye kughushi vyeti.

Dkt. Mpango ametaja mafanikio mengine kuwa ni ujenzi wa mradi wa umeme katika bonde la mto Rufiji, Stiegler’s Gorge, ambao ulikuwa ni moja ya ndoto za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,utakaozalisha MW 2100, kuimarisha usimamizi wa mapato ya ndani na kutoa elimu msingi bila ada.

Kuhusu mahusiano mazuri kati ya Serikali na walipa kodi, Waziri ameilekeza Mamlaka ya Mapato Nchini(TRA) kuchukua hatua za makusudi kuboresha mahusiano kati yake na walipakodi kwa lengo la kuondoa dhana iliyojengeka kuwa TRA inatumia vitisho kudai kodi.

Kwa kuzingatia kuwa uchumi wa watanzania wengi unategemea kilimo, Serikali imependekeza fedha nyingi zielekezwe katika kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, maghala na masoko, kuimarisha upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo. Kuhusu kilimo, pia huduma za ugani, kuboresha mfumo wa utafiti na utoaji wa matokeo hayo kwa wananchi na uendelezaji wa sekta ndogo za uvuvi na mifugo ni mambo yatakayopewa kipaumbele.

“Katika kuchochea ukuaji wa viwanda nchini, Serikali itaelekeza nguvu zake kwa kutekeleza Mpango wa Kuboresha Udhibiti wa Biashara ili kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi hususan viwanda vya nguo,ngozi na nyama, samaki, mafuta ya kula, madawa na vifaa tiba, vyakula vya binadamu na mifugo na katika sekta ya madini”, amesema Dkt. Mpango.

Bajeti hii imeweka vipaumbele vingine kwenye huduma za jamii kama vila upatikanaji wa maji safi na salama, kuendelea kugharamia elimu ya msingi na kuongeza idadi ya wataalam katika fani adimu kwenye maeneo ya mafuta na gesi, madaktari bingwa wa figo na moyo, pamoja na utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Serikali pia imependekeza msamaha wa kodi kwenye maeneo mbalimbali ili kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi. Maeneo hayo ni pamoja na kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye taulo za kike, jambo ambalo liliwafanya wabunge wengi hasa wanawake kumshangilia sana Mhe. Waziri.

Serikali inapanga kutumia jumla ya Shilingi trilioni 32.48, kati ya hizo trilioni 20.47 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na trilioni 12.01 kwa ajili ya maendeleo.

About Alex

Check Also

HA2

WAKULIMA KUSAJILIWA NA KUPATIWA VITAMBULISHO NCHINI

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akifungua  mkutano wa kitaifa wa wadau wa Tumbaku nchini leo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one + eleven =