Tuesday , March 26 2019

Home / MICHEZO / DAKIKA ZA MWISHO ZAIMALIZA TUNISIA KOMBE LA DUNIA DHIDI YA ENGLAND ‘KANE APIGA BAO MBILI’

DAKIKA ZA MWISHO ZAIMALIZA TUNISIA KOMBE LA DUNIA DHIDI YA ENGLAND ‘KANE APIGA BAO MBILI’

 

Harry Kane akishangilia kishujaa baada ya kuifungia mabao mawili England dakika za 11 na 90 na ushei katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Tunisia kwenye mchezo wa Kundi G Kombe la Dunia Jumatatu Uwanja wa Volgograd nchini Urusi. Bao la Tunisia limefungwa na Ferjan Sassi kwa penalti dakika ya 35 PICHA ZAIDI SOMA HAPA 

Ukisema matumaini ya Waafrika kwa wawakilishi wao watano wa Kombe la Dunia huko Urusi yamekuwa finyu, hautakuwa umekosea.
 
Tunisia imekuwa timu ya nne ya Afrika kupoteza mechi mechi ya kwanza na kesho ni zamu wa Senegal. Hata hivyo, Tunisia pia imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kufunga bao katika Kombe la Dunia 2018.
Sasa timu zote nne za Afrika zimecheza mechi ya kwanza na kupoteza baada ya mechi ya jana ya Tunisia ambayo ilifungwa na England, Harry Kane akifunga bao katika dakika ya 90.
Kabla ya Tunisia, timu tatu za Afrika zilishacheza na kupoteza na hakuna iliyofunga bao. Timu ya 5 ya Afrika ni Senegal, itacheza kesho dhidi ya Poland. Kumbuka hakuna iliyoshinda wala kupata sare katika mechi zote za kwanza.
Matumaini ya kuwa Senegal ni timu ya mwisho ya Afrika inayocheza leo kama kweli itaweza kuwabeba Waafrika na kuibua matumaini kama kweli kuna timu ya Afrika inaweza kusonga mbele.

Timu za Afrika zimekuwa zikifungwa  dakika za mwisho mwisho yaaani

Misri dakika 89
Morroco dakika 95
Tunisia dakika 91

MATOKEO:
Misri 0-1 Uruguay
Morocco 0-1 Iran
Croatia 2-0 Nigeria
England 2-1 Tunisia

About Alex

Check Also

Pix 2

RAIS WA TFF WALLACE KARIA AWASHUKURU WATANZANIA KUIUNGA MKONO TAIFA STARS

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) ametoa shukrani za dhati kwa Serikali,Taasisi Mbalimbali,Vyombo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 + 6 =