Tuesday , March 26 2019

Home / MICHEZO / WACHEZA GOLF ZAIDI YA 100 WATHIBITISHA KUSHIRIKI LUGALO OPEN

WACHEZA GOLF ZAIDI YA 100 WATHIBITISHA KUSHIRIKI LUGALO OPEN

press lugalo open

Mwenyekiti Lugalo Golf Club  Brigedia Jenerali Michael Luwongo katikati akiongea na Waandishi wa Habsari kuhusu Mashindano ya TANAPA lugalo open yanayotarajia kuanza Juni 22 Jijini Dar Es Salaam

Picha na Luteni Selemai Semunyu

………………..

Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ

Wachezaji zaidi ya 100 wa Mchezo wa Gofu kutoka vilabu mbalimbali nchini wamethibitisha kushiriki katika michuano ya mashindano ya Gofu ya Tanapa Lugalo open yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 22 katika Viwanja vya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania wa Lugalo Jijijini Dar es  Salaam.

Akizungumza katika mkutano wa Waandshi wa Habari Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwemo Uwanja na Zawadi ambazo kwa kawaida kutoka Lugalo huwa ni za kuvutia.

“Maandalizi yamekamilika na taarifa nilizonazo mpaka sasa wachezaji 100 wameshajiandikisha na muda bado upo hivyo nitoe wito kwa wachezaji wengine kujitokeza ili kushiriki katika Mashindano hayo ambayo yamekuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki na wachezaji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzani Joseph Tango aliipongeza Klabu ya JWTZ ya Lugalo kufuatia mchango mkubwa inaoutoa katika kuendeleza mchezo huo kwa kuanzi a na watoto na kuwa klabu ya Nyumbani kwa Mchezo wa Gofu.

Alisema mashindano hayo yatashirikisha  wachezaji wa Ridhaa na wa Kulipwa katika makundi yote ikiwemo Wanawake Wazee na Watoto sambamba na Wachezaji wasaidiizi ambao watapata nafasi katika Siku ya kwanza ya Mashindano.

Kwa Upande wake mwakilishi kutoka mamlaka ya Hifadhi za taifa TANAPA ambao ndi wadhamini wa mashindano hayo Juliana alisema wamejiandaa vyema na kila la muhimu linalohitajika katika kufanikisha mashindano hayo wameshatekeleza.

Aliongeza kuwa TANAPA kudhamini Gofu ni katika kuunga mkono Jitihada za Serikali kukuza michezo na gofu ina muunganiko na Utalii hivyo wanaimani kupitia Gofu pia itakuza uchumi kutokana na kukua kwa Utalii.

Mashindano ya  Lugalo open  hufanyika kila mwaka  kwa mujibu wa kalenda ya TGU na Klabu ya JWTZ ya Lugalo imekuwa ikipewa dhamana ya Kuyaaandaa.

About Alex

Check Also

Pix 2

RAIS WA TFF WALLACE KARIA AWASHUKURU WATANZANIA KUIUNGA MKONO TAIFA STARS

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) ametoa shukrani za dhati kwa Serikali,Taasisi Mbalimbali,Vyombo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − 5 =