Monday , February 18 2019

Home / MICHEZO / MGUU WA KAGERE WAIPELEKA SIMBA FAINALI KOMBE LA KAGAME,SASA KUKUTANA NA MABINGWA WATETEZI AZAM FC IJUMAA TAIFA

MGUU WA KAGERE WAIPELEKA SIMBA FAINALI KOMBE LA KAGAME,SASA KUKUTANA NA MABINGWA WATETEZI AZAM FC IJUMAA TAIFA

Meddie-Kagere-2

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya JKU ya Zanzibar jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba SC inakwenda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame na itakutana na Azam FC katika fainali Ijumaa hapa hapa Uwanja wa Taifa.
Kagere aliyesajiliwa mwezi uliopita kutoka Gor Mahia ya Kenya, alifunga bao hilo dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa ndani ya boksi baada ya kupokea pasi mshambuliaji Mghana, Nicholas Gyan anayetumika kama beki kwa sasa.
Pamoja na ushindi huo, Simba SC ilipata wakati mgumu kwa vijana wa Jesho la Kujenga Uchumi (JKU) waliokuwa wakiongozwa vizuri na kiungo hodari, Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Ikumbukwe katika Nusu Fainali ya kwanza, Azam FC ilishinda 2-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Taifa pia, mabao ya mshambuliaji mpya, Ditram Nchimbi dakika ya 92 na beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa dakika ya 100.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Pascal Wawa, Paul Bukaba, James Kotei, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk64, Mwinyi Kazimoto, Meddie Kagere, Mohammed Rashid/Moses KItandu dk89 na Marcel Kaheza/Rashid Juma dk78. 
JKU:  Mohammed Abrahman, Issa Haidar Dau, Edward Peter, Mwinjuma Mwinyi, Salum Said, Faisal Salum, Ali Vuai/Amour Suleiman dk58, Nassor Mattar, Abrahman Mussa, Suwed Juma na Khamis Abdallah.

About Alex

Check Also

9832670-6706055-image-a-15_1550177026096

CHELSEA YAPETA UGENINI EUROPA LEAGUE,YAICHAPA 2-1 MALMO

Ross Barkley na Olivier Giroud wakipongezana baada ya wote kuifungia Chelsea katika ushindi wa ugenini …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

8 − one =