Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / MKUU WA WILAYA YA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA ATOA MWEZI MMOJA KWA MADEREVA PIKIPIKI KUWA NA LESENI

MKUU WA WILAYA YA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA ATOA MWEZI MMOJA KWA MADEREVA PIKIPIKI KUWA NA LESENI

1

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akizungumz na waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kufungua mkutano wa madereva wa pikipiki  kwa ajili ya kukutana na wadau kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo kutokuwa na leseni, pamoja na kofia ngumu ili kuweka mikakati ya kuwasaidia pamoja na kupunguza wimbi la ajali ambazo zimekuwa zikijitokeza.

IMG_1259

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Wilaya ya Kibaha Edward Gontako akizungumza na wanahabari kuhusina na mikakati waliyojiwekea katika kuhakikisha wanapunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikipelekea kupoteza maisha ya watu

PICHA NA VICTOR MASANGU

……………….

VICTOR  MASANGU, KIBAHA

MKUU  wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama  ametoa muda wa mwezi mmoja  30 kwa madereva wote wa pikipiki  kuhakikisha wanakata na kuwa na leseni kwa lengo la kuweza kupunguza na kuondokana na  ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikipoteza maisha ya watu na nguvu kazi ya Taifa hususan kwa  vijana hao.

Agizo hilo amelitoa  wakati wa mkutano maalumu ambao aliuandaa kwa lengo la kuweza kuwakutanisha na wadau mbali mbali  wa maendeleo ili kuweza kusikiliza kero pamoja na kubaini changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili katika utekelezaji wa  majukumu yao ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Pia  katika hatua nyngine Mkuu huyo alibainisha kuwa  vijana wengine  ambao ni madereva  wa pikipiki katika Wilaya Kibaha wamekuwa wakivunja sheria mbali mba za barabarani ikiwemo kutokuwa na  hawana leseni  hivyo wanahatarisha usalama wa maisha yao pamoja na abiria ambao wanawapakia kwani kufanya hivyo ni kinyume kabisa na sheria za taratibu za barabarani.

“Kwa kweli kutokana na kuwepo kwa changamoto hii ya madereva wa pikipiki nimeamua kuitisha mkutano kwa ajili ya kuwakutanisha wadau mbali mbali wa maendeleo pamoja na taasisi mbali mbali ili kuwez kujadili kwa pamoja na kuweza kuona namna gani tunaweza kuwasaidia vijana hawa waweze kupata leseni pamoja na kuwezeshwa katika mikopo,”alisema Assumpter.

Nao madereva  hao wa pikipiki katizungumza katika mkutano huo wamesema kwamba kwa sasa wanakabiliwa na changamoto sugu ya kutokuwa na leseni,kofia ngumu pamoja na elimu ya kutosha kuhusiana na masuala mbali mbali ya sheria za barabarani hivyo kupelekea kusababisha kutokea kwa ajali ambazo zinapoteza uhai wa  maisha ya watu pamoja na majeruhi.

 Madereva hao akiwemo Ahmad Suleman  na a Said Issa   walisema kwamba kwa sasa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana kutokana na wakati mwingine wanajikuta wanatekwa na watu wasiofahamika na kuamua kuwawekea madawa ya kulevya na kuwafanyia vitendo vya kikatili  kisha kuwatupa maporini na kuondoka na pikipiki,huku baadhi ya wengine wakipoteza maisha yao.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa kuweza kuona kero yetu ya siku nyingi ya kuendesha vyombo vya moto bila ya kuwa na leseni,lakini kwa hiyvyo kutukutanisha na mamlaka zinazohusika tumeweza kupata elimu ya kutosha pamoja na jinsi ya kuweza kupatiwa taratibu zote za kuweza kupata leseni ambayo tutakuwa tunailipia kwa awamu,”walisema madereva hao.

 Naye Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Wilaya ya Kibaha Edward Gontako aliwataka kuhakikisha wanazingatia sheria zote za barabarani na kwamba wamejipanga vilivyo kwa ajili ya kuweza kutoa elimu na mafunzo mbali mbali ya sheria za usalama barabarani lengo ikiwa ni kuweza kupunguza ajali amabzo wakati mwingine zimekuwa zikisababisha na  uzembe  wa baadhi ya  madereva.

Isack Msemwa ni moja na wadau ambao walihudhulia katika mkutano ho ambaye pia msimamiSzi wa utoaji wa mikopo kutoka benki ya CRDB tawi la mbezi Jijini Dar es Salaam  alibainisha kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanaweka mikakati kabmbe ya kuwasaidia vijana ambao ni madereva pikipiki kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.

WILAYA ya Kibaha Mkoani Pwani kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa ikibabiliwa na changamoto kubwa ya kuwepo kwa baadhi ya madereva ambao wamekuwa wakiendesha vyombo hivyo vya moto bila ya kuwa na leseni  pamoja na kutovaa kofia ngumu,hali ambayo inahatarisha  kwa kiasi kikubwa usalama maisha yao.           

 

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × 1 =