Monday , December 10 2018

Home / MCHANGANYIKO / POLISI KILIMANJARO WAKAGUA LESENI YA MADEREVA 2000

POLISI KILIMANJARO WAKAGUA LESENI YA MADEREVA 2000

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP ,Hamis Issah akizungumza na madereva katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi wakati akifungua rasmi mafunzo kwa madereva hao ikiwa ni njia mojawapo ya kuwakumbusha Sheria ya Barabarani pamoja na matumizi ya Alama mpya za barabarani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah akiwaonesha Madereva baadhi ya Alama mpya ambazo zimeanza kutumika katika maeneo mbalimbali ya barabara.
Madereva wa Magari ya Abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wakati akizngumza nao katika kituo Kikuu cha Mabasi mjini Moshi.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ,ASP,Zauda Mohamed akimuonesha jambo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,ACP,Hamis Issah wakati alipokutana na madereva wa magari ya Abiria,Kulia ni Mkuu wa Operesheni wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,ACP,Costantine Maganga na kushoto ni Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani  mkoa wa Kilimanjaro,Ins,Peter Mizambwa.
Dereva mstaafu wa Magari makubwa ,Apolonary Malya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
JESHI la
Polisi mkoani Kilimanjaro limekagua Leseni za Madereva  2182 ,madereva 13
wakibainika kutumia Leseni za madaraja yasiyoruhusu kuendesha Magari ya Abiria
huku Madereva watatu wakishikiliwa kwa kosa la kuendesha gari bila ya kuwa
leseni.

 

 

Katika
ukaguzi huo uliofanyika kwa muda wa wiki moja katika mkoa wa Kilimanjaro ,Jeshi
la Polisi pi limebaini uwepo wa madereva waliovuka umri wa kuendesha gari kwa
mujibu wa sheria ambao ni miaka 60 huku likiwataka kuacha mara moja kuendelea
na kazi hiyo.

 

 

Kutokana na
mapungufu mbalimbali yaliyobainika kwa Madereva wa Magari ya Abiria ,Jeshi la
Polisimkoa wa Kilimanjaro likatangaza kuanza mafunzo kwa Madereva wa magari ya
Abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni
pamoja na maelekezo ya alama mpya za barabarani.

 

 

Akizungumza
kwa niaba ya Madereva,Dereva mzoefu wa magari makubwa ,Apolonary Malya
amepongeza utaratibu huo wa jeshi la Polisi kutoa mafunzo ikiwa ni sehemu ya
kuwakumbusha madereva baadhi ya sheria ya usalama barabarani.

 

 

Mafunzo kwa
madereva hao yameanza kutolewa katika ukumbi mdogo uliopo ofisi za kikosi cha
usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mkuu wa kikosi hicho Mrakibu
msaidizi wa Polisi Zauda Mohamed na maofisa wengine wa Polisi .

 

 

Mwisho .

About Alex

Check Also

4

KAMISHINA MASAIDIZI WA ARDHI KANDA YA MAGHARIBI AAGIZWA KUONGEZA NGUVU KATIKA CHUO CHA ARDHI TABORA

Brass Band ya Chuo cha Ualimu Tabora ikiongoza maandamano ya Wahitimu wa Chuo cha Ardhi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twelve − 5 =