Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / PROFESA MBARAWA AAGIZA DUWASA KUONGEZA MAKUSANYO

PROFESA MBARAWA AAGIZA DUWASA KUONGEZA MAKUSANYO

048A4443

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na Profesa Ahmed Ame, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Waziri alitoka kukagua mabwawa ya maji taka yaliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Wengine aliyeongozana nao ni Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Palangyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw. Athumani Shariff na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano DUWASA Bw. Warioba

048A4481

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akinawa mikono katika kisima kinachotoa maji bila kufungwa pump. Kisima hicho ni moja ya visima vilivyochimbwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) kwa ajili ya kupeleka maji katika mji wa serikali utakaojengwa Ihumwa. Waziri alikuwa katika ziara ya kukagua miradi inayosimamiwa na (DUWASA).

Profesa Mbarawa

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mbarawa akiwa na mtaalamu wa Maabara Jane Japhet akikagua ubora wa maji kwenye chanzo cha maji Mzakwe

……………….

Na: Fatuma Malende-Dodoma

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (Mb) ameagiza uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma (DUWASA) kuhakikisha kuwa kwa kipindi cha miezi sita waongeze ukusanyaji wa mapato kutoka 1.3 bilioni ya sasa hadi kufikia 1.8 bilioni.

Aidha, amewataka kuhakikisha wanapunguza upotevu wa maji ambao kwa sasa ni asilimia 28.7 ya maji yote yanayozalishwa na mamlaka hiyo.

“Hakikisheni upotevu wa maji unapungua ili kuongeza makusanyo kutoka 1.3 bilioni ya sasa mnayokusanya na kufikisha 1.8 bilioni miezi sita kuanzia sasa” Waziri alisema.

Waziri alisema upotevu wa maji ni mkubwa na maji yanayopotea ni mengi sana kama mnazalisha lita  milioni 48 na asilimia 28.7 zinapotea kiasi hicho ni kikubwa sana hivyo hakikisheni mnazuia upotevu huo.

Upotevu wa maji kwa sasa ni sawa na  lita milioni 16 kwa siku ambazo ni nyingi sana na ni hasara kwa shirika kwa kuwa serikali inapoteza pesa nyingi.  Hii ina maana kuwa kuna mahali yanapotea kutokana na uchakavu wa miundombinu au inawezekana kuna watu wamejiunganishia maji kiholela bila kufuata taratibu.

Akitoa ahadi katika mara baada ya kusikiliza taarifa ya Mamlaka, Waziri alisema serikali itahakikisha inatenga fedha ili kuongeza vyanzo na kuboresha miundombinu ya maji iliyopo ili kuweza kukidhi mahitaji ya jiji la Dodoma ikiwemo kutafuta vyanzo mbadala kwa ajili ya jiji la Dodoma ambapo sasa hivi idadi ya watu imeongezeka kutokana na Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi.

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

7 + nine =