Tuesday , March 26 2019

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

kamandamtei-620x308

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu na ajali za barabarani ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

Mnamo tarehe 11.07.2018 kuanzia majira ya saa 05:30 Alfajiri katika Stendi Kuu ya Mabasi iliyopo Kata ya Mbalizi Road, Tarafa ya Iyunga hapa Jijini Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya zoezi la ukaguzi wa Mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kwenda mikoa mbalimbali.

Aidha katika zoezi hilo lililofanywa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya sambamba na askari wa kikosi cha usalama barabarani, pia Jeshi la Polisi liliwafanyia kipimo cha ulevi madereva wa mabasi hayo kabla ya kuanza safari zao ili kujiridhisha juu ya utimamu wao afya.

Pia katika zoezi hilo baadhi ya mabasi yalikutwa na matatizo hivyo yalizuiliwa kuendelea na safari hadi pale wahusika watakapofanyia matengenezo. Kutokana na hilo Kamanda MATEI alizungumza na abiria wa mabasi husika ili kujua hali halisi ya chombo chao kabla ya kuanza safari.

Baada ya zoezi hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICH O. MATEI ametoa wito kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha Kamanda MATEI ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kufanyiwa kazi pamoja na kuendelea kutoa ushirikiano ambao utasaidia katika kuzuia uhalifu.

                    Imesainiwa na:

[ULRICH O. MATEI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

 

About Alex

Check Also

AA

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × 5 =