Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / TFS KUHIFADHI MISITU YOTE ILIYOMO NDANI YA JIJI LA DODOMA

TFS KUHIFADHI MISITU YOTE ILIYOMO NDANI YA JIJI LA DODOMA

deal-done-2

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo wakikabidhiana hati hati ya makubaliano inayoipa mamlaka TFS kupanda na kustawisha miti, na kuhifadhi misitu yote iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuikijanisha Dodoma mara baada ya wotw kusaini hati hiyo mapema hivi leo jijini Dodoma.

nasisitiza-dodoma-ya-kijani-inawezekana-na-hii-ni-ytekelezaji-wa-ILani

“Sisi kama Wakala wa Huduma za Misitu tumeshajipanga kuanza utekelezaji wa makubaliano haya na katika mwaka huu wa fedha takriban milioni 300 tumezitenga kwa ajili ya kuanza kutekeleza jukumu hili alisisitiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo kwa waandishi wa Habari (hawako pichani). Kushoto ni  Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi

prof-hapa-tunaweka

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo maeneo waliyokubalina katika hati ya makubaliano inayoipa mamlaka TFS kupanda na kustawisha miti, na kuhifadhi misitu yote iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuikijanisha Dodoma mara baada ya wotw kusaini hati hiyo mapema hivi leo jijini Dodoma.

saini-tunaweka

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo wakisaini hati ya makubaliano inayoipa mamlaka TFS kupanda na kustawisha miti, na kuhifadhi misitu yote iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuikijanisha Dodoma mapema hivi leo jijini Dodoma.

………………..

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imesaini hati ya makubaliano inayoipa mamlaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania- TFS ya kupanda na kustawisha miti, na kuhifadhi misitu yote iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuikijanisha Dodoma.

Dodoma imekuwa ni Halmashauri ya kwanza nchini kufanya Makubaliano ya aina hiyo yaliolenga kukabiliana na changamoto ya hali ya hewa na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015/2020 inayoelekeza serikali kuongeza eneo la kupanda miti kutoka hekta 60,000 mwaka 2015 hadi hekta 130,000 mwaka 2020.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi wakati akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kusainiana makubaliano hayo jijini humo leo.    

“Siku ya Leo tumefanya jambo la kihistoria na wenzetu Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS, kama mnavyojua Dodoma ni mji mkuu wa Serikali, kama jiji tumeona tuna changamoto ya hali ya hewa na niwashukuru TFS kuona jambo hili ni la muhimu,

“Tumeingia mkataba wa makubaliano kwamba TFS watahifadhi misitu yote iliyoko ndani ya Jiji la Dodoma na kama haitoshi katika maeno yote tutakayopimwa kama hifadhi ya ardhi kwa ajili ya kupanda miti watapanda miti na maeneo yote ya vilima ndani ya jiji la Dodoma watayahudumia kwa kuwa kwa mujibu wa sheria maeneo hayo hayamilikishi hivyo ni mali ya serikali, lakini na maeneo yote yenye vyanzo vya maji kwa maana ya mita 60 kutoka kwenye mabwawa ya maji TFS watayahudumia,” alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo anasema jiji la Dodoma limekuwa na ongezeko kubwa la watu linalosababisha ongezeko la shughuli za kiuchumi ambazo zinahitaji mifumo mizuri ya kimazingira ili kukabiliana na hali yoyote inayoweza kusababishwa na maongezeko hayo.

Professa Silato anasema ni kwa sababu hiyo wameamua kuchukua jukumu la kuhakikisha mifumo ya kiikolojia inakuwepo salama kwa mana ya kuwepo kwa uoto wa kijani, uoto wa miti na mimea katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha kwamba wakazi wa Dodoma wanaishi katika mazingira ambayo yana afya.

Professa anaongeza kuwa watahuhisha Jiji la Dodoma kwa kuanza kupanda miti maeneo ambayo yameonekana kuharibika au hayakuwa na uoto huku maeneo ambayo yanaonekana kuhitaji kuhifadhiwa ili kurudi kwenye uoto wake kuyahifadhi na katika kutekeleza hayo wamekubaliana na jiji kutafuta rasilimali fedha, rasilimali watu na vifaa vya kutekeleza kazi hiyo.

“Sisi kama Wakala wa Huduma za Misitu tumeshajipanga kuwa na rasilimali watu, tumejipanga kuwa na usafiri maalum kwa ajili ya kazi hii lakini pia fedha ambapo katika mwaka huu wa fedha takriban milioni 300 tumezitenga kwa ajili ya kuanza kutekeleza jukumu hili! Fedha hizi zinaweza kuwa kidogo lakini kwa kuwa tunashirikiana na jiji tutaangalia ni wapi tunaweza kupata fedha zaidi na pale itakapoonekana zinahitajika rasilimali zaidi ya hizi nilizosema basi tuko tayari kuziongeza ili tufikie malengo kwa haraka zaidi na kwa spindi ambayo kila mtu anaitarajia,” anasema Professa Silayo.

Meneja wa Kanda ya Kati ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Mathew Kiondo anayesimamia moja kwa moja utekelezaji wa makubalianao hayo anasema kanda yake itahakikisha inasimamia kikamilifu utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayolenga kulinda rasilimali za misitu na kuboresha mazingira.

 

About Alex

Check Also

IMG_06055

RAIS DKT.SHEIN AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYA KASKAZINI B, UNGUJA

      RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen − 3 =