Thursday , January 17 2019

Home / MCHANGANYIKO / HALMASHAURI TENGENI MAENEO YA UWEKEZAJI ILI REA III IWAJENGEE MIUMNDO MBINU YA UMEME –DKT KALEMANI

HALMASHAURI TENGENI MAENEO YA UWEKEZAJI ILI REA III IWAJENGEE MIUMNDO MBINU YA UMEME –DKT KALEMANI

1

Mkuu wa Wilaya wa Sikonge Peres Magiri akizungunza na wakazi wa Kijiji cha Kisanga jana wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa uwashaji wa umeme baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu chini ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

2

Mbunge wa Jimbo la Sikonge ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR –TAMISEMI) Joseph Kakunda akizungunza na wakazi wa Kijiji cha Kisanga jana wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa uwashaji wa umeme baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu chini ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

3

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungunza na wakazi wa Kijiji cha Kisanga jana wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa uwashaji wa umeme baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu chini ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

4

Baadhi ya wanakijiji wa Kisanga wilayani Sikonge wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nishati (hayupo katika picha) jana wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa uwashaji wa umeme baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu chini ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

5

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani(kulia) akimkabidhi jana Mbunge wa Jimbo la Sikonge ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR –TAMISEMI) Joseph Kakunda (kushoto) kifaa kinajulikana kama umeme tayari (UMETA) kwa ajili ya kugawia baadhi ya wazee ili nao waweze kupata umeme unaotokana na utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

7

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akikata utepe jana katika Kijiji cha Kisanga wilayani Sikonge wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa uwashaji wa umeme baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu chini ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

8

Baadhi ya wanakijiji wa Kanyamsenga wilayani Sikonge wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nishati (hayupo katika picha) jana wakati akiwahutubia na kuwaahidi kuwapelekea umeme chini ya chini ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

9

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwaongoza viongozi mbalimbali kutoa zawadi kwa wanakwaya wa kijiji cha Kanyamsenga wilayani Sikonge kabla ya kuwahutubia na kuwaahidi kuwapelekea umeme chini ya chini ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

 

Picha na Tiganya Vincent

RS TABORA

………….

NA TIGANYA VINCENT

RS TABORA

SERIKALI imezitaka Halmashauri za Wilaya hapa nchini kutenga maeneo ya uwekezaji wa aina mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda ili wakati utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) ili uweze kujenga miundo mbinu ya umeme katika maeneo hayo kwa Wawekezaji.

Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Sikonge na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa ujenzi miundo mbinu ya umeme wa kupitia REA III na kuwasha umeme katika kijiji cha Kisanga.

Alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha anapopatikana Mwekezaji wa kujenga  Viwanda, hoteli na maeneo mengine akute miundo mbinu ya umeme tayari pio katika eneo hilo ili asitumie muda mrefu kusubiri kuwekewa umeme baada ya kukamilisha ujenzi.

“Tunataka kila Halmashauri zote ambazo umeme wa REA awamu ya tatu unatekelezwa zianishe maeneo ya uwekezaji ili wakati Wakandarasi wanajenga mradi wa kusambaza umeme kwa wananchi na maeneo hayo yawekewe miundo mbinu ya umeme…hii itasaidia kuwavutia hata wawekezaji wa kujenga viwanda katika Halmashauri zet” alisema.

Katika hatua nyingine Waziri huyo wa Nishati amesema kuanzia sasa uunganishaji wa umeme katika maeneo yote ya vijijini hautakiwi kuzidi shilingi 27,000/- hata kama baadhi ya wanakijiji waliunganishiwa umeme na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)

Waziri alitoa agizo hilo kufuatia kilio cha wananchi wa Kijiji vya Pangale na vingine kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri na Mbunge wa Jimbo la Sikonge Joseph Kakunda kusema kuwa wamekuwa wakiunganishiwa umeme wa kiwango cha shilingi 177,000/- na TANESCO wakati wako vijijini.

Walidai kuwa kiwango hicho ni kikubwa na wamekuwa wakidai kinaonyesha ubaguzi kwa baadhi ya vijiji kulipa 27,000/- kuunganishiwa umeme wa REA na kwa wale amabo waliunganishiwa kupitia TANESCO kutozwa kiasi 177,000 wakati nao wako vijijini.

Akijibu hoja hizo alisema wakazi wote wa vijijini wawe waunganishiwa umeme na Tanesco au REA watalipa 27,000/- kupata huduma hiyo na sio zaidi ya hapo.

Wakati huo huo Waziri wa Nishati amewaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya hapa nchini kuhakikisha Taasisi zote za umma zinaunganishwa na umeme wa REA III kabla ya kumalizika kwa utekelezaji wa mradi huo.

Alisema majengo yote ya umma kama vile Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati, Shule na Ofisi za Vitongoji, Vijiji na Kata lazima ziunganishwe na umeme huo ili yaweze kutoa huduma kwa wananchi kwa ufanisi zaidi.

Dkt. Kalemani alisema Wakurugenzi wanatakiwa kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha wanaunganishiwa maeneo hayo na umeme huo.

Aidha aliwataka wananchi wote hapa nchini ambao mradi unatekelezwa kuchangammkia fursa ya kuunganisha nyumba zao na  umeme wa REA awamu ya Tatu muda huu wa ambapo gharama bado ziko chini kwani baada ya mradi kumalizika wanaweza kuunganisha kwa gharama kubwa.

Aidha Waziri huyo amemuagiza Mkandarasi anayotekeleza mradi wa REA III kuhakikisha anapeleka umeme katika  bwawa la Uluwa wilayani Sikonge ambacho ni chanzo cha maji kwa wakazi wapatao 20,000 wa vijiji 8.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuwapatia wananchi hao maji ya uhakika baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kushindwa kutokana gharama kubwa ya uendeshaji wa Jenereta ya milioni 12 ili kuzalisha maji kwa mwezi.

Alisema matumizi ya Jenereta yanaipa Halmashauri hiyo gharama kubwa ambapo haiwezi lakini kwa kutumia umeme wa REA watapunguza

About Alex

Check Also

HA2

WAKULIMA KUSAJILIWA NA KUPATIWA VITAMBULISHO NCHINI

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akifungua  mkutano wa kitaifa wa wadau wa Tumbaku nchini leo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twelve − nine =