Sunday , October 21 2018

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TUME YA MADINI

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TUME YA MADINI

ngao

TAARIFA KWA UMMA

Tume ya Madini kwa Mujibu wa Kanuni Namba 6(2)(b) ya The Mining (Local Content) Regulations, 2018 inawataka waombaji na wamiliki wote wa leseni za utafutaji, uchenjuaji, uyeyushaji, usafishaji na uchimbaji mkubwa na wa kati wa madini kuwasilisha Mpango wa Ushirikishwaji wa Utoaji Huduma na Bidhaa kwa wazawa katika Miradi ya Madini. Kutokana na Kifungu cha 106(3) cha Sheria ya Madini, Tume pia inawataka waombaji na wamiliki wa leseni hizo kuwasilisha tamko la Kiapo cha Uadilifu (Integrity Pledge). Miongozo ya nyaraka hizo inapatikana katika tovuti ifuatayo:- www.tumemadini.go.tz na www.madini.go.tz. Kwa vile uchambuzi wa maombi umeshafanyika, hivyo utoaji wa leseni hizo utafanyika pindi tu waombaji watakapowasilisha nyaraka tajwa.

Atlikult Imetolewa na:

Prof. Idris Kikula MWENYEKITI Julai 17, 2018

About Alex

Check Also

3

Matukio Katika Picha Tamasha la Wajasiriamali wanawake Jijini Dodoma

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akisisitiza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one × two =