Sunday , October 21 2018

Home / MCHANGANYIKO / WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI MTEULE WA KENYA HAPA NCHINI

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI MTEULE WA KENYA HAPA NCHINI

Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.). Mara
baada ya kuwasilisha nakala hizo Mhe. Mahiga na Balozi Kazungu walipata fursa ya kuzungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya hususan kwenye sekta za biashara, uchumi na elimu.
Tukio hilo lilifanyika kwenye Ofisi Ndogo ya Wizara iliyopo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Julai, 2018. 
Dkt. Mahiga akiendelea na mazungumzo na Balozi Mteule wa Kenya hapa nchini
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Kenya nchini. Kushoto ni Bibi Judica Nagunwa na Bw. Magabilo Murobi
Balozi Kazungu akimweleza jambo Dkt. Mahiga
Mazungumzo yakiendelea kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Kazungu
Picha ya pamoja.
Dkt. Mahiga akiagana na Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania. 
About Alex

Check Also

3

Matukio Katika Picha Tamasha la Wajasiriamali wanawake Jijini Dodoma

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akisisitiza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × one =