Monday , February 18 2019

Home / MICHEZO / FAINALI YA MDAHALO KWA SHULE ZA SEKONDARI TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA 2018

FAINALI YA MDAHALO KWA SHULE ZA SEKONDARI TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA 2018

1

Mwakilishi wa shule ya Sekondari ya Londoni iliyopo mjini Songea-Ruvuma, Hellena Pilla akipokea tuzo kutoka kwa mgeni rasmi Mbunge wa Songea Mjini, Dr. Damas Ndumbaro baada ya shule yake kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya mdahalo kwa shule za sekondari, ulioandaliwa na Taasisi ya SOMI kupitia Tamasha la Majimaji Selebuka, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Songea.

2

Mgeni rasmi katika mashindano ya mdahalo kwa shule za sekondari ulioandaliwa na Taisisi ya SOMI, Mbunge wa Songea Mjini, Dr. Damas Ndumbaro akimkabidhi zawadi ya mpira wa kikapu uliotolewa na Benki ya NMB, mwakilishi wa shule ya Sekondari ya Londoni iliyopo mjini Songea-Ruvuma, Hellena Pilla iliyoshika nafasi ya kwanza.

3 (1) 3 (2) 3 (3)

Mwafunzi bora kipengele cha uwasilishaji bora katika mashindano ya mdahalo kwa shule za sekondari ulioandaliwa na Taasisi ya SOMI kupitia  Tamasha la Majimaji Selebuka, Elda Simwaba wa Shule ya Peramiho Girls akipokea tuzo kutoka kwa mgeni rasmi Dr. Damas Ndumbaro mbunge wa Songea Mjini, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Songea, Ruvuma Julai 19.

4

Mwanafunzi Oscar Ngonzi wa Shule ya Pehimisco, aliyeibuka mchoraji bora wa vibonzo katika shindano la uchoraji lililoandaliwa na Tamasha la Majimaji Selebuka, akipokea tuzo kutoka kwa Mbunge wa Songea Mjini, Dr. Damas Ndumbaro aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, kwenye Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Songea, Julai 19.

5

Mwanafunzi Mwanaidi Mbunde  wa Shule ya Maposeni, aliyeshika nafasi ya pili katika shindalo la uchoraji vibonzo lililoandaliwa na Tamasha la Majimaji Selebuka, akipokea tuzo kutoka kwa Mbunge wa Songea Mjini, Dr. Damas Ndumbaro aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, kwenye Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Songea, Julai 19.

6 (1) 6 (2)

  1. Nasma Ally, mwanafunzi  wa Shule ya Sekondari ya Daora kutoka Dar es Salaam akipokea zawadi kutoka kwa Mbunge wa Songea Mjini, Dr. Damas Ndumbaro katika kipengele cha wawasilishaji bora (best presenter) kwenye mashindano ya mdahalo kwa shule za sekondari uliondaliwa na Taasisi ya SOMI kupitia tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Songea Julai 19.

7

  1. Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Londoni, Jordan Sanga akipokea zawadi ya mshindi katika kategoria ya Mwalimu Bora kutoka kwa Mbunge wa Songea Mjini, Dr. Damas Ndumbaro aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya mdahalo kwa shule za sekondari ulioratibiwa na Taasisi ya SOMI kupitia tamasha la Majimaji Selebuka, hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Songea mkoani Ruvuma, Julai 19.

NA MWANDISHI WETU, SONGEA

 

SHULE ya Sekondari Londoni iliyopo Lizaboni mjini Songea Mkoa wa Ruvuma imeibuka vinara wa jumla katika mashindano ya Mdahalo ‘Debating’ yaliyoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Songea-Mississippi (SOMI), kupitia tamasha la Majimaji Selebuka.

Shindano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Songea mkoani Ruvuma ambako Mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Damas Ndumbaro na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA), na Benki ya NMB waliokuwa wadhamini.

Mada shindaniwa ilikuwa ni faida na hasara za ulipaji kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki ‘EFD’s’.

Katika kipengele hicho cha Ushindi wa Jumla ‘Best School Over All’, Londoni ilifuatiwa na Sekondari ya Ruhuwiko huku nafasi ya tatu ikishikwa na Songea Boys.

Kipengele cha Uwasilishaji Bora ‘Best Presentation School’ Songea Girls waliibuka washindi wakifuatiwa na Peramiho Girls huku nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Daora kutoka jijini Dar es Salaam.

Wawakilishi Bora ‘Top 5 Best Presenters’ waliopenya ni Elda Simwamba kutoka Peramiho Girls ambaye alikuwa kinara, Yusto Mwaiginsya kutoka Sekondari ya De Paul, Faines Msola wa Songea Girls, Nasma Ally wa Daora na Christandus Mhagama kutoka Luwawasi Sekondari.

Pia kulikuwa na shindano la uchoraji vibonzo, ambako Oscar Ngonzi wa Sekondari ya Pehisco aliibuka mshindi akifuatiwa na Mwanaidi Mbunde wa Maposeni huku nafasi ya tatu ikienda kwa Sharifa Makarani wa Sekondari ya Londoni.

Washindi walizawadiwa zawadi mbalimbali ikiwamo tuzo, fedha taslimu, vifaa vya kitaaluma na kimichezo, kufunguliwa akaunti benki ya NMB na kuwekewa kianzio.

Aidha,  walimu waliofanikisha shule zao kufanya vizuri walikabidhiwa zawadi za fedha taslimu.

Akizungumza kabla ya Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo, aliwapongeza waandaaji na washiriki, kwani wanatoa mchango mkubwa katika kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa jamii.

“Waandaaji wangeweza kulenga kitu kingine, lakini wameamua kuandaa mada hii, tunawashukuru kwani wanajenga walipa kodi wajao…Wengi wetu tumelikuta hili ukubwani ndio maana unaona kuna ukakasi kwa baadhi ya watu katika kulipa kodi,” alisema na kuongeza.

Lakini jamii ikijengewa uelewa na kuelewa faida za ulipaji kodi itasaidia serikali katika ukusanyaji wa kodi na kufanikisha kuendesha shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi, Dk. Ndumbaro, mbali na kuwapongeza washiriki na kuwataka kuwa mabalozi wema katika kutoa elimu juu ya faida ya ulipaji kodi.

Dk. Ndumbaro, alibainisha kuwa tofauti kubwa ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea na ufanyaji kazi na ulipaji kodi.

“Nchi haiwezi kuendelea bila kufanya kazi, kwenye wanafunzi kazi kubwa ni kusoma kwa bidii na pia kushiriki stadi za mikono…Wenzetu nchi zilizoendelea wanachapa kazi sana na kulipa kodi zinazojenga nchi na nyingine tunazoenda kuomba misaada, lakini sisi ni wavivu na visingizio vingi katika kazi na kutoona umuhimu wa kulipa kodi,” alisema Dk. Ndumbaro.

Aidha, alisisitiza kuwa ulipaji kodi ni uchumi hivyo asiyelipa kodi ni adui wa maendeleo na anapaswa kupigwa vita.

Dk. Ndumbaro ambauye pia ni Mkurugenzi mwenza wa SOMI, aliwapongeza TRA na NMB na kwamba tamasha la mwakani litakalofanyika kuanzia Julai 13-21 kwa upande wa mdahalo mada itaendelea kuwa ulipaji kodi katika maeneo mengine zaidi ya mashine za kielektroniki iliyokuwepo mwaka huu.

 

About Alex

Check Also

9832670-6706055-image-a-15_1550177026096

CHELSEA YAPETA UGENINI EUROPA LEAGUE,YAICHAPA 2-1 MALMO

Ross Barkley na Olivier Giroud wakipongezana baada ya wote kuifungia Chelsea katika ushindi wa ugenini …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × two =