Friday , October 19 2018

Home / MCHANGANYIKO / WATU 18 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA

WATU 18 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA

rpc nley

NA TIGANYA VINCENT

TABORA

POLISI Mkoa wa Tabora linawashikiria watu 18 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuwachoma moto na wengine kushiriki katika mauaji.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Emmanuel Jackson .

Alisema watuhumiwa 16 wanashikiriwa kwa tuhuma cha kujaribu kuwaua wanawake wanne kwa kuwachoma moto.

 

Kamanda huyo alisema  wananchi kwa kushirikiana na Polisi wa wilaya ya Kaliua waliweza kuwaokoa wanawake hao  wanne waliokuwa wamekamatwa na walinzi wa jadi zaidi ya miambili.

Kamanda Jackson alisema kuwa julai 16 mwaka huu saa nne usiku huko
msitu wa Hifadhi ya Isawima kata ya Igwisi wilaya ya Kaliua kiongozi
wa  Sungusungu aitwaye Ingese Irea akiwaongoza wenzake 200 na
kuwakamata akinamama wanne.

Alisema kuwa watu hao waliwakamata akinamama  hao waliotambuliwa kwa majina ya Velediana Paulo (70), Modesta Magazi (45), Joyce Elias Magazi (33) na Nyamizi Dotto (40) walitaka kuwaua wakiwatuhumu kuwa ni wachawi.

Kamanda huyo aliongeza kuwa watuhumiwa hao na wenzao ambao bado wanasakwa baada ya kuwakata wakina mama hao walikusanya kuni nyingi na kisha kuwasha moto kwa dhumuni la kuwachoma.

Jackson alisema kuwa wakati watuhumiwa wakiendelea na za
kufanikisha unyama huo taarifa toka kwa wananchi wema zilifika Polisi
ambao bila kukawia walifika eneo la tukio na kuwaokoa na kufanikiwa kuwakamata baadhi yao.

Matukio ya aina hii ambayo yameegemea kwenye imani za kishirikina
yanaendelea kushamiri katika vijiji mbali mbali vya mkoa wa Tabora
hasa ambako wanaishi jamii ya wafugaji wa kabila la Wasukuma na kuupa  mkoa sifa mbaya.

Mwishoni mwa mwaka uliopita watu wengine 55 wakazi wa kata ya Loya wilaya ya Uyui mkoani hapa akiwemo mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho walikamatwa baada ya jaribio lao la kutaka  kuwaua wakina mama wanne kwa kuwachoma moto kwa imani hizo hizo kushirikana.

Wakati huo huo jeshi la Polisi linamshikiria  Maganga Machibya (22) anayetuhumiwa kumuua Edina Mayunga  mkazi wa kijiji cha Ifumba Wilaya ya Nzega kwa kumkata shingo kutokana na imani za kishirikina.

Katika tukio jingine la mauaji Abdalah Salehe mkazi wa Ipuli Manispaa
ya Tabora anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mkewe Regina Athuman kwakumpiga na kisha kumnyonga

About Alex

Check Also

images

MWAKYEMBE APOKEA KWA MASIKITIKO TAARIFA YA KIFO CHA MTANGAZAJI ISAAC GAMBA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fifteen − three =