Wednesday , December 12 2018

Home / MICHEZO / UBAGUZI WA RANGI NA DHARAU KUTOKA CHAMA CHA DFB,OZIL ASTAAFU RASMI KUICHEZEA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI

UBAGUZI WA RANGI NA DHARAU KUTOKA CHAMA CHA DFB,OZIL ASTAAFU RASMI KUICHEZEA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI

_102647336_555e26a1-b9b2-4146-8b41-b5e229259a7a

Mesut Ozil amejiondoa kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani akisema amestaafu kwa sababu ya UBAGUZI WA RANGI na DHARAU kutoka kwa Chama cha Soka Ujerumani (DFB) na mashabiki.

Ozil mwenye asili ya Uturuki amekuwa akituhumiwa kuonyesha kiwango duni wakati wa Kombe la Dunia nchini Urusi ambako Ujerumani ilivuliwa ubingwa.

Hadi anatangaza kustaafu soka la kimataifa, Ozil ameichezea Ujerumani mechi 92, amefunga mabao 23.
Aliisaidia kubeba Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Mwaka 2012 walifika nusu fainali ya Euro na 2016 wakabeba ubingwa.

Alianza kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani mwaka 2009 na 2010 alikuwa katika kikosi kilichoshiriki Kombe la Dunia kama 2018.

About Alex

Check Also

index

DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA DISEMBA 15,2018

Dirisha Dogo la Usajili kwa Klabu za Ligi Kuu,Daraja la Kwanza na Daraja la Pili …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

thirteen + 1 =