Saturday , November 17 2018

Home / MCHANGANYIKO / GOFU LUGALO YAWASILI NA KUANZA VYEMA MUFINDI OPEN

GOFU LUGALO YAWASILI NA KUANZA VYEMA MUFINDI OPEN

LUGALO KUWASILI MUFINDI 1

Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Golf ya Lugalo wakiwasili katika uwanja wa Gofu wa Mufindi mkoani Iringa yenye lengo la Kutangaza vivutio vya Utalii vya nyanda za juu kusini  hususani Mufindi.

GEOFREY LEVERIAN MUFINDI 2

Mchezaji gofu wa kulipwa kutoka Klabu ya Lugalo Geofrey Leverian aliyeibuka mshindi kwa kupiga mpira Mrefu akipiga  Mpira wakati wa Mashindano ya wazi ya Mufindi yenye lengo la Kutangaza vivutio vya Utalii vya nyanda za juu kusini  hususani Mufindi.

Na Luteni Selemani Semunyu

Wachezaji wa klabu Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo imewasili salama Mufindi Mkoani Iringa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya wazi ya mufindi  ya utalii karibu Kusini Mufindi gofu challenge yanayotarajiwa kuanza kesho(leo) kwa wachezaji wa ridhaa..

Akizungumza mara baada ya kuwasili Afisa Utawala wa klabu ya Lugalo Kapteni  Amanzi  Mandengule alisema timu imewasili salama na hakuna majeruhi na siku ya leo wataitumia kwa ajili ya mazoezi ili kuufahamu uwanja.

“ Tumefika salama na Timu yetu sote tukiwa salama na Wachezaji wetu wa Kulipwa wameingia uwanjani leo ikiwa ndio siku yao na tunaimani tutafanya vizuri pia kwa kundi hilo” Alisema Kapteni Mandengule.

Kapteni Mandengule aliongeza kuwa  licha ya kuwa wamefika salama lakini kuna changamoto ya hali ya hewa kwani  Mufindi ni baridi ukilinganisha na Dar es Salaam ambapo hali nin ya Joto lakini watapambana kwa kuwa walilifahamu hilo

Kwa upande wa wachezaji wa kulipwa wachezaji 11 wameingia uwanjani kumenyana katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa iringa kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii yakilenga kutangaza fursa na vivutio vya utalii nyanda za juu kusini.

Katika hatua ya mwanzo ya michuano hiyo Mchezaji  George Leverian wa Lugalo ameibuka na ushindi kwa kupiga mpira mrefu na wameingia katika Raundi ya pili itakayoamua mshindi katika vipengele vingine na ushindi wa Jumla.

Katika mashindano hayo ya siku tatu mbali na kushiriki katika mashindano hayo lakini watapata fursa ya kutembelea na kujifunza masuala mbalimbali kuhusu sekta ya utali hususani utalii wa nyanda  za juu kusini.

Mbali na wachezaji wa kutoka Klabu ya Lugalo pia Wachezaji kutoka Vilabu vya Morogoro Gymkhana,  Dar es Salaam Gymkhana, Moshi Club  ,TPC, Kili Golf Club ya Arusha  na wenyeji klabu ya Mufindi  ya Iringa  watashiriki katika mashindano hayo.

About regina

Check Also

IMG_5910

MAZOEZI YA PAMOJA YA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAMEWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akizungumza wakati akifunga kufunga …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 + 12 =