Wednesday , April 24 2019

Home / BIASHARA / TIGO YATOA MILIONI 10 KWA MSHINDI WA PROMOSHENI YA TIKISA NYAVU

TIGO YATOA MILIONI 10 KWA MSHINDI WA PROMOSHENI YA TIKISA NYAVU

IMG_7010

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa jumla katika promosheni ya ujumbe mfupi wa maneno ya Tikisa Nyavu iliyoendana na msimu wa soka la kimataifa, Godfrey Njau wa Dar es Salaam (kulia). 

IMG_7091

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya zawadi ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa jumla katika promosheni ya ujumbe mfupi wa maneno ya Tikisa Nyavu iliyoendana na msimu wa soka la kimataifa, Godfrey Njau wa Dar es Salaam (kulia). Katikati ni Mtaalam wa Huduma za Ziada wa Tigo, Fabian Felician.

……………….

Dar es Salaam,

Tigo Tanzania imemzawadia Godfrey Njau (28), mkaazi wa Dar es Salaam anayejishugulisha na  biashara ya kutoa na kusafirisha bidhaa donge nono la shilingi milioni 10, baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya ujumbe mfupi ya Tikisa Nyavu.

Huku shangwe za tukio kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018 zikiwa zimefikia kikomo, kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali ya Tigo imemtangaza Godfrey kuwa mshindi wa promosheni hiyo iliyoendana na uzinduzi wa tovuti ya Tigo ya michezo www.tigosports.co.tz

‘Mbali na kitita cha TZS 10 millioni, washindi wengine walijinyakulia zawadi nne za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine wanne wakijishinda luninga za kisasa na watano wakizawadiwa simu janja,’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema alipokuwa akikabidhi zawadi kwa mshindi jijini Dar es Salaam leo.

Kupitia tovuti ya michezo ya Tigo, Watanzania walipata fursa ya kufurahia uhondo wa tukio kubwa zaidi ya mpira wa miguu kwa mwaka 2018 kwa nguvu ya mtandao mkubwa zaidi wa 4G nchini. Wateja pia walipokea habari na dondoo muhimu kuhusu shindano hilo kubwa zaidi la mpira wa miguu kwa mwaka 2018. Kwa kujisajili kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wateja  wa Tigo walipata fursa ya kushiriki katika shindano la ujumbe mfupi wa maneno ambapo mshindi wa kitita cha shilingi milioni kumi alipatikana.

‘Tigo inajivunia kuwaletea Watanzania matukio yote ya mchuano mkubwa zaidi wa mpira wa miguu kwa mwaka 2018 moja moja kwenye simu zao za mkononi, huku wakifurahia huduma bora za kidigitali kwa gharama nafuu za intaneti kwenye mtandao mkubwa zaidi wa 4G nchini. Hii inaendana na sifa kuu ya Tigo ya kuwaelewa wateja na kubuni bidhaa na huduma bora zinazoendana na mahitaji yao,’ Woinde aliongeza.

……………………………………………………………………………………………………………….

Kuhusu Tigo:

Tigo Tanzania www.tigo.co.tz ni kampuni ya simu inayotoa huduma bora za maisha ya kidigitali nchini Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995.

Kupitia huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi. Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali. Ni kampuni ya kwanza Tanzania kuzindua facebook na smartphone zenye lugha ya Kiswahili, huduma ya TigoPesa, pamoja na kuzindua huduma ya kwanza iliyowezesha wateja kufanya miamala ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki.

Tigo ni kampuni ya simu ya pili kwa ukubwa nchini na kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, imekuwa kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini. Kupitia mkakati mkubwa wa kupanua na kuboresha huduma zake, kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Tigo  ilizindua mtandao wa 4G LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine 22 nchini.

Tigo inajivunia jumla ya watumiaji milioni 11 wa simu waliosajiliwa, na imetoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zile zisizokuwa na moja kwa moja kwa Watanzania wapatao 300,000; hii ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.

Tigo ni nembo ya kibiashara ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya maisha ya kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za kibiashara katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini, Ofisi kuu za Millicom zipo Ulaya na Marekani.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana na: woinde.shisael@tigo.co.tz

 

About Alex

Check Also

IMG-20190422-WA0031

MBUNGE VULLU NA DAU WATOA MSAADA WA VIFAA MAFIA

NA MWAMVUA MWINYI,  Mafia   MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Pwani ,Zaynabu Vullu, ametoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × 4 =