Saturday , November 17 2018

Home / Uncategorized / WANARIADHA POLISI WAAGWA, WATAKIWA KUTANGULIZA UZALENDO

WANARIADHA POLISI WAAGWA, WATAKIWA KUTANGULIZA UZALENDO

Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha

Timu ya riadha ya Polisi imeagwa jana mchana na kuondoka leo kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya Michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (EAPCCO GAMES).

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Afisa Mnadhimu wa Jeshi hilo mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Yusuf Ilembo aliwataka askari hao kutanguliza uzalendo kwa Jeshi la Polisi na nchi kwa ujumla hivyo wajitume kwa uwezo wao wote ili waweze kuibuka na ushindi mnono.

“Ingawa tuna wawakilishi katika michezo mbalimbali lakini Jeshi la Polisi lina mategemeo makubwa juu ya mchezo wa riadha hivyo naimani mtachukua medali zote na hatimaye kuwa washindi”. Alisema Afisa Mnadhimu huyo.

Wanariadha hao Kumi na Nane walioweka kambi kwa muda wa miezi sita eneo la Ilboru wilaya ya Arumeru watashiriki Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza tarehe 06 Agosti jijini Dar es saalam kwa kukimbia mbio ndefu na mbio za kati.

Akizungumzia maandalizi ya kambi hiyo, Msimamizi wa Michezo toka Shule ya Mafunzo ya Polisi Moshi, Inspekta Emmanuel Mtatifikolo alisema wana matumaini makubwa ya kushinda nafasi za juu na hawataliangusha Jeshi la Polisi japokuwa kuna nchi tishio kama vile Kenya na Uganda.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Riadha mkoa wa Arusha Fredy Shahanga alisema kwamba, kwa kipindi chote chama chake kimekuwa kikishirikiana na kambi ya Jeshi hilo na kuhakikisha kunakuwepo na mazingira mazuri kwa wachezaji huku akijinasibu kwa kusema kwamba timu hiyo itafanya vizuri na kuiletea sifa nchi yetu.

Mbali na Riadha michezo mingine inayotarajiwa kuchezwa ni pamoja na Karate, Judo, Boxing, Mpira wa Pete, Mpira wa Mikono Mpira wa Miguu, Taekwondo na Kulenga Shabaha.

Mashindano hayo ya EAPCCO yanayoshirikisha jumla ya nchi Nane kwa mwaka huu yalianza rasmi tarehe 8 Desemba 2017 nchini Uganda ambapo Tanzania ilikuwa Mshindi wa Tatu na mwaka huu Tanzania imekuwa mwenyeji  na lengo kubwa la Mashindano hayo ni kudumisha Ushirikiano na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa kazi  kwa askari wa nchi hizo.

Pichani Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Yusuf Ilembo akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha hao pamoja na viongozi wa Polisi ngazi ya mkoa (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)

About regina

Check Also

ZZZZZZZZZZZZZZZZZ

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

  KUVUNJA HOTEL USIKU NA KUIBA. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eleven + 1 =