Wednesday , April 24 2019

Home / MICHEZO / TAIFA STARS YAPATA KOCHA MPYA KUTOKA NIGERIA

TAIFA STARS YAPATA KOCHA MPYA KUTOKA NIGERIA

38391559_287922401984851_1989880209620336640_n

Emmanuel Amunike (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo hoteli ya New Africa mjini Dar es Salaam

……………..

Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amemtambulisha winga wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, Emmanuel Amunike kuwa kocha mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars.
Karia amemtambulisha Amunike mwenye umri wa miaka 47 katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika hoteli ya New Africa mjini Dar es Salaam jioni hii baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Amunike aliyeng’ara na Super Eagles katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 nchini Marekani akicheza wingi ya kushoto, mtihani wake wa kwanza utakuwa ni mchezo dhidi ya Uganda Septemba 8, mwaka huu mjini Kampala, kabla ya kuwafuata Cape Verde Oktoba 10 kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Taifa Stars inakuwa timu ya kwanza ya taifa ya wakubwa Amunike kufundisha, baada ya awali kuwa kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kwao, Nigeria kuanzia mwaka 2014 hadi 2017.
Zaidi ya hapo, Amunike mwenye umri wa miaka 47 amefundisha klabu za Al Hazm ya Saudi Arabia, kama Kocha Msaidizi mwaka 2008 kabla ya kuhamia Julius Berger hadi mwaka 2011 alipojiunga na Ocean Boys, zote za Nigeria.
Alipoachana na U-17 ya Nigeria akaenda kufundisha Al Khartoum SC ya Sudan kuanzia mwaka 2017 hadi 2018 na sasa anakuja kuujaribu ‘mfupa’ uliowashinda wengi, Taifa Stars.  
Kisoka, Amunike aliibukia klabu ya Concord mwaka 1990 kabla ya kwenda kuchezea Julius Berger 1991, zote za kwao, Nigeria baadaye Zamalek ya Misiri mwaka 1991 hadi 1994 ndipo akahamia Ulaya.
Alianza na klabu ya Sporting CP ya Ureno kuanzia 1994 hadi 1996 kabla ya kuhamia Barcelona ambako alicheza hadi mwaka 2000 alipohamia Albacete zote za Hispania na mwaka 2003 alijiunga na Busan I’Cons ya Korea Kusini alikocheza hadi 2004 akahamia Al-Wehdat ya Jordan kumalizia soka yake.

About Alex

Check Also

1

Wizara ya Habari yawasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2019/20

 Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × five =