Saturday , November 17 2018

Home / MICHEZO / RC MAKONDA ATEMBELEWA NA RAIS WA TFF, WAWEKA MIKAKATI THABITI YA KUIMARISHA MICHEZO

RC MAKONDA ATEMBELEWA NA RAIS WA TFF, WAWEKA MIKAKATI THABITI YA KUIMARISHA MICHEZO

IMG-20180807-WA0156
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelewa ofisini kwake na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia na Mwenyekiti wa Michezo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamefanya mazungumzo ya kuimarisha sekta ya Michezo.
Miongoni mwa mambo waliyozungumzia ni Suala la heshima iliyopata Tanzania kuwa mwenyeji wa Michuano ya Mashindano makubwa ya michezo kwa Jeshi la Polisi katika nchi za mashariki na Kati zikihusisha Nchi Saba ambapo tayari michuano hiyo imefunguliwa rasmi siku ya Jana na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Aidha wamezungumzia maandalizi ya mashindano makubwa ya CECAFA, CAF kwaajili ya michuano ya AFCON yakihusisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 yanayotaraji kufanyika August 11 Mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa yakijumuisha mataifa 10 Afrika.

IMG-20180807-WA0066

RC Makonda amesema michuano yote hiyo itafanyika Jijini Dar es salaam na kwakuwa inahusisha ugeni kutoka mataifa mbalimbali itatoa fursa kwa wananchi wa Dar es salaam hususani wenye hotel, vyakula, usafiri na wafanyabiashara kupata kipato kupitia mashinano hayo.
Kwa upande wake Rais wa TFF Wallance Karia amempongeza RC Makonda kwa jitiada za kuinua sekta ya michezo kupitia ujenzi wa uwanja wa Bandari ambapo amesema wameamua kumuomba ushirikiano kwakuwa wanaamini uwezo ukubwa alionao kwenye kusimamia jambo na kufanikisha.

About Alex

Check Also

images

RT yamtambulisha mkufunzi kutoka Japan

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), jana limemtambulisha Mkufunzi wa kujitolea kutoka nchini Japan, Ayane Sato. …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × 5 =