Saturday , November 17 2018

Home / Uncategorized / WAZIRI DKT.KALEMANI AIPA “KONGOLE” TANESCO, MWEKEZAJI AIFAGILIA SERIKALI

WAZIRI DKT.KALEMANI AIPA “KONGOLE” TANESCO, MWEKEZAJI AIFAGILIA SERIKALI

 

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (kulia), na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kamel Group, wamiliki wa Kamel Industrial Estate, Bw.Gagan Gupta, wakitembelea eneo la EPZA la Kamel Industrial Estate huko Bagamoyo Mkoani Pwani Agosti 6, 2018.

 

NA
MWANIDHI WETU
WAZIRI
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, na mwekezaji wa Kampuni ya Kamel Group, Bw.
Gagan Gupta, wamelipongeza Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), kwa kuharakisha
uwekaji umeme mkubwa kwenye eneo la EPZA Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Pongezi
hizo zimetolewa Agosti 6, 2018 wakati Mhe. Dkt. Kalemani alipofika kwenye eneo
hilo la uwekezaji viwanda (Kamel Industrial Estate), lililoko kandokando ya Barabara
ya Bagamoyo Wilayani humo.
“Niipongeze
TANESCO kwa sababu imechukua muda mfupi sana tangu ulipolalamika, takriban
miezi miwili kazi ya kufikisha umeme hapa imekamilika, na ilikuwa ni kazi
kubwa, umeme wa kiwanda hiki ulikuwa una –share
na watumiaji wengine wengi, 33kV uki-share
na watu wa Bagamoyo, watu wa Tegeta, kwa mtu wa kiwanda usingekutosha.”
Alisema.
Alisema
TANESCO baada ya kupokea malalamiko hayo kazi ya kuongeza kiasi cha umeme
kwenye kiwanda hicho ilianza kwa kufunga mitambo hapo hapo kiwandani, ambapo
umeme ulivutwa kutoka unapoanzia Mkoa wa Pwani kuelekea Bagamoyo.
“Tumeamua
kukuwekea laini yako peke yako, kutoka pale Mkoa wa Pwani unapoanzia na kuleta
umeme hapa, na kisha tumeuingiza kwenye transfoma yako, tumeingiza 33kV kwa
ajili yako yenye uwezo wa kutumia Megawati 22, ingawa umetuambia mahitaji yako
ni Megawati 20, sisi tumekuletea ziada ya Megawati 2 hivyo ni matumaini yetu
sasa kero itapungua na uzalishaji utaongeza.”
Alisema
ni matumaini ya Serikali kuwa kiwanda kitazalisha zaidi ya Mitungu 500
iliyokuwa ikizalisha kwa siku kwani hivi sasa umeme upo wa kutosha.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Bw. Gagan Gupta alisema, amefurahi
sana kupelekewa umeme wa kutosha moja kwa moja kwenye kiwanda chake na kwamba
ameahidi kuwa uzalishaji mkubwa utafanyika ndani ya kipindi kifupi kijacho.
“Kwangu
mimi leo ni siku ya kihistoria, Mhe. Waziri uko hapa ninakuahidi katika nia hii
ya serikali ya kuweka uchumi wa viwanda, ninachoweza kusema, ongezeko la Megawati
20 moja kwa moja hapa kiwandani, ndani ya mwaka mmoja utakuta mabadiliko makubwa
hapa.” Alitoa hakikisho Bw. Gupta.

 

 

 

Mhe. Waziri akimsikiliza Bw. Gupta kuhusu mipango ya uwekezaji viwanda kwenye eneo hilo
Mhe. Waziri akimsikiliza Bw. Gupta kuhusu mipango ya uwekezaji viwanda kwenye eneo hilo
Mhandisi Mahende Mgaya, (Kulia), akimpatia maelezo Mhe. Dkt. Kalemani kwenye eneo ambalo TANESCO imetengeneza laini pekee ya kuelekea moja kwa moja eneo la EPZA la Kamel Industrial Estate.
Dkt. Kalemani akizungumza na Bw. Gupta alipowasili kwenye eneo hilo.
Mhe. Dkt. Kalemani, akimpongeza Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mgaya. Kulia ni Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu

About regina

Check Also

ZZZZZZZZZZZZZZZZZ

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

  KUVUNJA HOTEL USIKU NA KUIBA. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 − four =