Tuesday , March 26 2019

Home / MICHEZO / MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI YAENDELEA KUSHIKA KASI DAR

MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI YAENDELEA KUSHIKA KASI DAR

2 (4)

Na. Jeshi la Polisi.

 Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO)  imeendelea kupamba moto huku Tanzania ikiwa imepata medali ya dhahabu katika mbio za mita 5000,Fedha moja na Shaba tano katika mchezo wa Karate.

Mwanariadha Fabian Nelson ndiye aliyefungua pazia kwa kuipatia Tanzania medali ya dhahabu baada ya kuwapita wenzake kutoka Kenya ambao walipata medali za fedha na Shaba.

Matumaini makubwa kwa Tanzania yapo katika mchezo wa kulenga shabaha, Judo,  Mpira wa Miguu na Riadha kwa upande wa mbio ndefu ambapo wanariadha wanaoshiriki michezo hiyo wameonyesha kiwango kikubwa.

Nahodha wa timu ya kulenga Shabaha Tanzania Inspekta  Noel seng’ng’e, amesema mchezo huo umekuwa mzuri kwani wameweza kutoa wachezaji wengi wazuri katika kulenga shabaha na wanaimani ya kuibuka na ushindi wa jumla katika mchezo huo.

Kwa Upande wake Kocha wa Timu ya Mpira wa Miguu John Tamba amesema vijana wake wako vizuri na morali ipo juu hasa ukizingatia ushindi walioupata katika mchezo wa awali baada ya kuichapa Polisi Uganda mabao 2 kwa 1.

“Mchezo unaofuata tunacheza na Rwanda hivyo tumefanya mazoezi mepesi ili kuhakikisha kuwa tunaibuka na ushindi utakaotufanya tuendelee kuongoza katika mpira wa miguu na hatimaye kuchukua ubingwa” Alisema Tamba.

Hata hivyo nchi za Rwanda, Kenya  na Uganda nazo zimeonyesha ushindani mkubwa baada ya kunyakua ushindi katika Mchezo wa Karate na mbio fupi huku wakiendelea kuchukua alama katika mpira wa mikono, pete na Karate.

Michezo inayoshindaniwa mwaka huu ni pamoja na soka ,mpira wa mikono, mpira wa wavu, mpira wa pete, Ngumi, Taekwondo, Judo na Riadha ambapo inafanyika katika Uwanja wa Taifa kwa riadha na michezo mingine inafanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

 

About regina

Check Also

Pix 2

RAIS WA TFF WALLACE KARIA AWASHUKURU WATANZANIA KUIUNGA MKONO TAIFA STARS

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) ametoa shukrani za dhati kwa Serikali,Taasisi Mbalimbali,Vyombo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × 5 =