Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / JAFO AAGIZA MAFISADI BIHARAMULO WASHUGHULIKIWE

JAFO AAGIZA MAFISADI BIHARAMULO WASHUGHULIKIWE

      Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiongea na wananchi wa Nyakanazi Mkoani
Kagera.


 Baadhi ya vifaa kwaajili ya kituo cha afya Nyakanazi ambavyo vitawekwa katika kituo
cha afya Nyakanazi

 Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na usalama wa wilaya ya
Biharamulo wakimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo eneo la Nyakanazi Mkoani Kagera.

     
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ameliagiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo kuijadili taarifa ya uchunguzi ya upotevu wa mapato katika Halmashauri hiyo. 

 Uchunguzi huo umetokana na Kamati ya fedha ya Halmashauri hiyo kuunda timu ya uchunguzi ili kubaini upotevu katika ukusanyaji wa mapato. 

 Waziri Jafo amefanya ziara hiyo leo Biharamulo akitokea Geita baada ya Halmashauri hiyo ya Biharamulo iliyopo mkoani Kagera Kushindwa kufikia malengo kwa kukusanya asilimia 60 huku kukiwa na taarifa za ubadhirifu wa mapato.

 “Kuna ubadhirifu wa kiwango kikubwa mpaka Kamati ya fedha ikaamua kuunda timu ya uchunguzi, niwaagize Baraza kukaa na kuwachukulia hatua watakaobainika kwenye hili ikiwa ni pamoja na kuwapeleka katika vyombo vya sheria,”amesema. 

 Katika hatua nyingine, Waziri Jafo ametembelea Kituo cha Afya Nyakanazi ambacho kilipata Sh.Milioni 500 za ukarabati. 

 Jafo ameridhishwa kwa kazi kubwa iliyofanywa kituoni hapo na kuwapongeza wananchi kwa ushirikiano wao uliowezesha kukamilika kwa miundombinu hiyo. 

 Aidha Waziri Jafo ameendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kigoma kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo. 

About regina

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − eight =