Monday , February 18 2019

Home / SIASA / KAMPENI ZA ‘LALA SALAMA’ WABUNGE WA CCM WATIKISA BUYUNGU

KAMPENI ZA ‘LALA SALAMA’ WABUNGE WA CCM WATIKISA BUYUNGU


               Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akiteta jambo na Mbunge wa
Vitimaalum Matha Mlata 

                    

 wananchi wakiwa kwenye kampeni za CCM zikiendelea katika
Jimbo la Buyungu.

 Baadhi ya Wabunge wa CCM pamoja na makada mbalimbali katika
moja ya mikutano ya kampeni jioni ya leo.

 Mbunge
wa Kisarawe Selemani Jafo akiwa na baadhi ya makada wa CCM katika kampeni
wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

Mbunge wa Vitimaalum Mary Chatanda akiwa na viongozi
mbalimbali katika harakati za kampeni za Jimbo la Buyungu.

                            ……………………………………………………………………………………….


 Wakati zimebaki siku mbili za kampeni kabla ya uchaguzi wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko Mkoani Kagera kufanyika, Wabunge wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wameonekana kunogesha kampeni hizo kwa hoja mbalimbali wakimdani mgombea Ubunge wa Jimbo hilo wa chama hicho Mhandisi Christopher Chiza. 


 Katika kampeni za leo wabunge wa CCM waliokuwa wakimwaga Sera kwa wananchi ni pamoja na Peter Serukamba, Selemani Jafo, Matha Mlata, Joseph Msukuma, Josephine Genzabuke, Ashantu Kijaji, na Mary Chatanda.

Wabunge wengine ambao wamekuwa katika kampeni hizo kwa nyakati tofauti ni pamoja na Nape Nnauye, Livingstone Lusinde, Hussein Bashe, na aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara ambao wamekuwa wakimwaga Sera za CCM ili kukiletea ushindi chama chao.


 Wakizungumza katika kampeni hizo, Wabunge hao wamewahakikishia wananchi wa Kakonko kwamba watampa ushirikiano wa kutosha mgombea huyo watakapokuwa pamoja bungeni katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zikiwemo hospitali ya wilaya, vituo vya afya pamoja na miundombinu ya barabara. 


 Aidha wamewaasa wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu.

About Alex

Check Also

L4

NGEMELA LUBINGA AFUNGUA MKUTANO WA KUPOKEA MAONI YA WANACCM NA WATANZANIA JUU YA MUSWADA WA VYAMA VYA SIASA JIJINI DAR ES SALAAM.

 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa- Chama Cha Mapinduzi,Ngemela Lubinga, akifungua mkutano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

20 − 15 =