Sunday , October 21 2018

Home / MCHANGANYIKO / KIWANDA CHA TBL ARUSHA CHATOA MSAADA WA PRINTER OFISI YA KATA YA THEMI

KIWANDA CHA TBL ARUSHA CHATOA MSAADA WA PRINTER OFISI YA KATA YA THEMI

PRINTER DONATION 2

Meneja wa kiwanda cha TBL Arusha,Joseph Mwaikusa(wa pili kutoka kulia) akikabidhi Printer ya kisasa kwa watendaji wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Themi.

PRINTER DONATION 4

Watendaji wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Themi wakipokea Printer mashine iliyotolewa na TBL.

Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia kiwanda chake cha Arusha,imetoa msaada wa Printer ya kisasa kwa ajili Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Themi,iliyopo mkoani humo kwa ajili ya kurahisisha kazi za kuwahudumia wananchi.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi mashine hiyo,Afisa Mtendaji wa kata ya Themi,Sophia Masinde,alishukuru kwa msaada huo ambao alisema utarahisisha kuhudumia wananchi wa kata  hiyo wanaofika ofisini hapo kupata huduma mbalimbali.”Tunashukuru kampuni ya TBL kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye maeneo ambayo mnafanyia biashara zenu”alisema Masinde.
Kwa upande wake,Meneja wa kiwanda cha TBL cha Arusha,Joseph Mwaikusa,alisema msaada huo  ni moja ya jitihada za kampuni kujitoa kusaidia changamoto mbalimbali na kujenga uhusiano na wadau mbalimbali nje ya kampuni.
Tunayo furaha  kutoa msaada huu,moja ya sera ya kampuni yetu ni  kuwaleta watu pamoja na kuwawezesha kuishi vizuri katika ulimwengu Maridhawa, hivyo tunatambua umuhimu wa  kushiriki kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii iliyotuzunguka”.Alisema Mwaikusa.

About regina

Check Also

3

Matukio Katika Picha Tamasha la Wajasiriamali wanawake Jijini Dodoma

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akisisitiza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fifteen + 19 =