Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / MEYA MWITA ATEMBELEA HOSPITAL YA AGA KHAN JIJINI HAPA LEO

MEYA MWITA ATEMBELEA HOSPITAL YA AGA KHAN JIJINI HAPA LEO

MSTAHIKI  Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amefanya ziara katika hospitali ya Aga Khan ya jijini hapa  na kuwaona wagaonjwa sambamba  na kupata nafasi ya kuona maendeleo ya mradi wa upanuzi wa hospitali hiyo ulio mbioni kukamilika .

Katika ziara hiyo , Meya Mwita amekutana na uongozi wa juu wa Hospitali hiyo ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utoaji Huduma za Afya Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki,  Sulaiman Shahabuddin ambapo walipata nafasi ya kuzungzumza mambo mbalimbali.

Meya Mwita ameipongeza Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan Tanzania kwa kuamua kuwekeza katika Mkoa wa Dar es Salaam hususani sekta ya Afya ambapo bado changamoto ni nyingi jijini  hapa pamoja na nchi nzima.

Aidha Meya  Mwita amefarijika  kuona hosipitali hiyo  imewekeza katika vifaa tiba vya kisasa zaidi kuwemo nchini pamoja na uwepo wa Watanzania wengi  katika eneo la utoaji huduma za viwango vya juu kabisa Tanzania.

Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za Huduma za Afya Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki  Sulaiman Shahabuddin amemshukuru Meya Mwita kwa kutenga muda wake na kutembelea hospitali hiyo.

Amefafanua kuwa “ni faraja kwetu sana kukuona mahali hapa Mstahiki Meya ,Hospitali hii ni kwa ajili ya Wana Dar es Salaam na Watanzania wote, Ninacho mshukuru Mungu ni kuona hospitali hii sasa ikianza kuhudumia hata mataifa ya jirani kama Comoro, Zambia, Malawi, Msumbiji ” amesema.

” Sisi tumedhamiria kuendelea kuwekeza katika eneo la Afya kwa kiasi kikubwa na hadi sasa ukiachilia mbali ujenzi wa hospitali hii ulio gharimu takribani shilingi bilioni 192 za Kitanzania unaokwenda sambamba na uwekaji wa vituo vya Afya 35 nchi nzima ambamo katika mkoa wa Dar es Salaam pekee hadi sasa tuna idadi ya vituo 11 vinavyofanya kazi na kuendeshwa kisasa kupitia mifumo ya kiteknolojia na mawasiliano kuwezesha uwepo wa huduma bora kabisa” ameongeza.
 
Awali Meya Mwita aliahidi kushughulia chamgamoto mbalimbali za nje ya hosipitali ikiwepo kuwapatia kibali maalum cha Ujenzi wa Daraja la juu ili kuvusha watu kutoka upande wa maegesho ya magari hospitalini hapo kwenda eneo la majengo ya hospitali,.

Aidha aliahidi kufutilia upatikanaji wa kibali kwa hosipitali hiyo kujenga maegesho ya kisasa ya magari kwa aajili ya wagonjwa eneo la ufukwe wa bahari ya Indi,  kufuatilia tozo za maegesho eneo lilijengwa na hosipitali na kuzindoa rasmi kama sehemu ya makusanyo ya jiji kwani hilo litawasaidia madaktari na wahudumu katika hosipitali kuongeza morali na ufanisi katika utendaji.

Sambamba na hilo  Mstahiki Meya ameahidi kushughulia kwa pamoja maboresho ya eneo la mbele ya hosipitali hiyo kwa kushirikiana na hosipitali kutafuta namna mbadala ya kuwasadia wenye biashara ndogondogo katika eneo kuendesha katika hali ya ubora zaidi.

Katika ziara hiyo Meya Mwita aliambatana na Mbunge wa jimbo la Vunjo  James Mbatia  na kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi ya Afya Aga Khan Tanzania ambapo alionekana kufuruhishwa na kasi ya maendeleo ya ukuaji wa huduma za afya nchini hasa kwa Aga Khan kuweza kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha ili kuboresha mifumo ya utaoji huduma za Afya kwa nchi nzima.

About regina

Check Also

3

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 30

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza na wajumbe wa kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

14 − 8 =