Monday , February 18 2019

Home / SIASA / WAGOMBEA 26 WAJITOKEZA KUIRITHI MIKOBA YA RAIS KABILA

WAGOMBEA 26 WAJITOKEZA KUIRITHI MIKOBA YA RAIS KABILA

ramadhani

Mgombea wa chama tawala nchini Kongo PPRD, Emanuel Shadari anayeungwa mkono na Rais Joseph Kabila.

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Kongo imeorodhesha majina ishirini na sita ya wagombea urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika orodha hiyo, wagombea huru waliojitokeza katika kinyang’anyiro hicho ni 16 wakati wa vyama wakiwa 8 ambapo kati yao wapo wanawake watatu na mawaziri wakuu wa zamani nchini humo 3.

Miongoni mwa wagombea 8 wa upinzani ni pamoja na Jeanpierre Bemba, Vital Kamerhe na Felix Tshisekedi kiongozi wa chama cha UDPS. Wagombea watatu ni wanawake ambao wawili wameishi ugenini akiwemo bi Monique Mukuna.

Antoine Gizenga ,mwenye umri wa miaka 94,waziri mkuu wa zamani na pia mshirika wa zamani wa rais Kabila ni mgombea pia wa kiti cha urais. Kuna pia mawaziri wakuu wa zamani 2 Adolphe Muzito na Samy Badibanga ambao ni wagombea pia.

Chanzo: D.W Swahili

About regina

Check Also

L4

NGEMELA LUBINGA AFUNGUA MKUTANO WA KUPOKEA MAONI YA WANACCM NA WATANZANIA JUU YA MUSWADA WA VYAMA VYA SIASA JIJINI DAR ES SALAAM.

 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa- Chama Cha Mapinduzi,Ngemela Lubinga, akifungua mkutano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

8 + 9 =