Sunday , October 21 2018

Home / MCHANGANYIKO / WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS ISSA HAJI USSI(GAVU)AONGOZA UJUMBE WA ZANZIBAR KATIKA KIKAO NA WATAALAMU WA NCHI ZA FALME ZA KIARABU(UAE)

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS ISSA HAJI USSI(GAVU)AONGOZA UJUMBE WA ZANZIBAR KATIKA KIKAO NA WATAALAMU WA NCHI ZA FALME ZA KIARABU(UAE)

DSC_1161

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi  akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza Mkutano uliowakutanisha  Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  na  Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za Falme za Kiarabu kuhusiana na mambo mabalimbali  na sekta mbalimbali ambazo wanaweza kusaidia mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyyat Shangani mjini Zanzibar. 

DSC_1154

Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE)Reem Ibrahim Alhashimy  akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza Mkutano   uliowakutanisha Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi na  Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za Falme za Kiarabu kuhusiana na mambo mabalimbali  na sekta mbalimbali ambazo wanaweza kusaidia mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyyat Shangani mjini Zanzibar.

DSC_1074

Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE)Reem Ibrahim Alhashimy wapili kushoto akizungumza katika mkutano uliowakutanisha  Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za Falme za Kiarabu kuhusiana na mambo mabalimbali  na sekta mbalimbali ambazo wanaweza kusaidia mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyyat Shangani mjini Zanzibar.

DSC_1070

Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (kushoto)wakiwa wamekutana na Ujumbe wa Wataalamu kutoka Nchi za Falme za Kiarabu Ukiongozwa na Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE)Reem Ibrahim Alhashimy wakijadiliana mambo mbalimbali na sekta mbalimbali ambazo wanaweza kusaidia mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyyat Shangani mjini Zanzibar.

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

Serikali ya Falme za kiarabu (UAE) inatarajia kufungua Ubalozi wake mdogo Zanzibar kabla ya kumalizika Mwaka 2018 ikiwa ni mwendelezo wa kuimarisha mahusiano ya kidugu katika nchi hizo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi na Ushirikiano wa Kiamataifa wa UAE, Reem Ibrahim Alhashimy alipozungumza na Wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa majadiliano kati ya Viongozi wa Serikali ya Zanzibar na UAE ukumbi wa Hotel ya Park Hyyat Mjini Zanzibar.  

Amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo kutazidisha mashirikiano yaliyopo na kuongeza kasi ya utekelezaji wa yale yaliyokubaliwa baina ya nchi hizo mbili.

Waziri Reem amesema madhumuni ya kuja Zanzibar ni kuihakikishia Serikali na Wananchi wa Zanzibar kwamba UAE ipo tayari kutekeleza yale yaliyoahidiwa katika Ziara ya Dkt Shein iliyofanyika nchini humo mwanzoni mwa mwaka huu.

Amesema kwa muda mrefu Wananchi wa UEA wamekuwa wakitembelea Zanzibar na kuwekeza katika maeneo mbali mbali kutokana na mahusiano mema yaliyojengeka miaka mingi.

“Binafsi sio mara ya kwanza kuja Zanzibar nimekuwa nikitembelea kutokana na uzuri wa Zanzibar  na watu wake na hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kushirikiana katika mambo yetu” alisema Reem

Sekta muhimu ambazo Serikali ya ya UAE imeonesha nia ya kuisaidia Zanzibar ni pamoja na Sekta ya Afya, Kilimo na Miundombinu.

Hata hivyo hakuainisha zaidi ni eneo gani kati ya Bandari na Uwanja wa ndege ambalo UAE wataweza kuisaidia Zanzibar.

Kwa upande wake Wanziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu amesema ziara hiyo imefungua matumaini makubwa kwa Zanzibar na kwamba itasaidia Zanzibar kujikwamua kiuchumi.

Amesema mbali na miradi iliyoombwa na Serikali ya Mapinduzi kwa UAE nchi hiyo pia ipo tayari kuisaidia Zanzibar katika miradi mingine ya ziada, ikiwemo uwezeshaji wa Vijana ili kukabiliana na tatizo la ajira.

Timu hiyo ya Wataalam iliwasili jana na kufanya Mikutano mbalimbali ya majadiliano na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa ahadi mbalimbali zilizotolewa katika ziara ya Dkt. Shein aliyoifanya January mwaka huu katika Falme za Kiarabu.

About regina

Check Also

3

Matukio Katika Picha Tamasha la Wajasiriamali wanawake Jijini Dodoma

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akisisitiza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five × one =